HAPA NDIPO ILIPOFIKIA MAHAKAMA YA MAFISADI
SERIKALI imewahakikishia Watanzania
kuwa mchakato wa kuanzishwa kwa Mahakama Maalumu ya mafisadi na wezi,
umefikia hatua nzuri. Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe
alisema hayo juzi bungeni mjini hapa, wakati akichangia Hotuba ya Rais
ya Ufunguzi wa Bunge.
Akizungumzia mchakato wa kuanzishwa kwa
mahakama hiyo maalumu, Mwakyembe alisema unakwenda vizuri na
utakapokamilika Watanzania watafahamishwa. “Kiongozi wa Serikali ya
Awamu ya Tano, akitoa tamko lazima litekelezwe.
Kama tunakumbuka Rais, kwa nyakati
tofauti kipindi cha kampeni, aliahidi kuanzisha Mahakama Maalumu ya
Mafisadi na Wezi,” alisema Mwakyembe. Akiizungumzia hotuba ya Rais,
Mwakyembe alisema ikiachwa hotuba ya Mwalimu Nyerere, ya Magufuli pia ni
bora na iligusa mioyo ya Watanzania wenye nia njema na Taifa.
“Wakati rais anatoa hotuba yake
iliyokuwa na aya 160, alipigiwa makofi na vigelegele mara 137, ni zaidi
ya asilimia 86, ya Dk Martin Luther ambaye ni Mmarekani mweusi,” alisema
na kuongeza kuwa hatua hiyo, imewaweka pabaya wapinzani waliokuwa
wanapinga kila kitu.
Dk Mwakyembe alisema tatizo ni kwamba
kwa hotuba hiyo, yeyote akijaribu kuipinga, wananchi watamuona wa hovyo.
Aliendelea kusema; “Wamejaribu (upinzani) kutoka kwenye mjadala, kwa
hoja tu ya TBC (Shirika la Utangazaji Tanzania), ili wasiwepo kwenye
mjadala, kwani wakiwepo lazima wataisifia tu.”
Post a Comment: