Dk. Salim Ahmed Salim :jumuiya za kimataifa zilishtushwa na uamuzi huu wa kufuta uchaguzi
Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, ameshangazwa na
uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta uchaguzi visiwani
humo.
Amesema jumuiya za kimataifa zilishtushwa na uamuzi huo,
amesema kinachotakiwa hivi sasa ni haki itendeke kwa kila kila upande
kukaa na kutafuta suluhisho la kudumu. “Tanzania haijazoea migogoro ya
siasa jambo ambalo si jema katika sura ya kimataifa,” alisema.
Mwanadiplomasia huyo wa kimataifa ametoa kauli hiyo,baada
ya Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, kutangaza kufuta matokeo ya
uchaguzi huo Oktoba 28, mwaka jana. Alisema hatua ya kufutwa uchaguzi
wa Zanzibar ni jambo lililowashangaza wengi kwa kuwa uchaguzi
ulifanyika kwa amani na utulivu, huku waangalizi wa ndani na nje
wakiusifia katika ripoti zao. “Ni hatua ambayo imewashangaza
wengi…imeibua sintofahamu kubwa katika nchi yetu kwa sababu uchaguzi
uliopita Tanzania ilipata sifa,baada ya uchaguzi kufanyika kwa amani na
utulivu. Lakini kitendo cha kufutwa kumewashangaza wengi na bado suala
hili halieleweki. “Pia hili jambo sidhani kama ni la mtu mmoja…sidhani
kama ni la Jecha peke yake. Huu si mustakabali mzuri kabisa, Zanzibar ni
nchi ndogo, lakini ina historia kubwa kisiasa hivyo juhudi za pamoja
zifanyike kutatua mgogoro huu kwa matakwa ya Watanzania kwa ujumla.
Post a Comment: