Washukiwa wa bomu bandia ndege ya Air France wakamatwa Ufaransa
MAOFISA wa Polisi nchini Ufaransa wamewatia mbaroni abiria wawili wa
ndege hiyo ambao ni mke na mme liokuwa abiria katika ndege ya Air France
Boeing 777 nambari AF463 iliyolazimika kutua kwa dharura nchini Kenya
hapo jana kufuatia tishio la bomu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Air France alifutilia mbali
tahadhari ya bomu iliyosababisha ndege hiyo ya kutua kwa dharura Kenya
na kusema kuwa lilikuwa bomu bandia.
Frederic Gagey aliwaambia waandishi wa habari mjini Paris, Ufaransa
kuwa kifaa kilichodhaniwa kuwa kilipuzi kilikuwa ni mbao na kisanduku
cha karatasi tu wala hakikuwa na uwezo wowote wa kuhatarisha usalama wa
ndege hiyo.
Inasemekana kuwa abiria mmoja alikipata kifaa hicho chooni na akamfahamisha mhudumu mmoja wa ndege hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria 459 na wahudumu 14.
Mhudumu huyo alimfahamisha rubani kuhusiana na kifaa hicho na shughuli za kutua kwa dharura zikaanza.
Ndege hiyo ilitua saa sita usiku wa kuamkia Jumapili, huku wataalamu
wa kutegua mabomu kutoka jeshi la wanamaji la Kenya wakiingia ndani ya
ndege hiyo kukagua kifurushi kilicholeta taharuki.
Sasa kitengo cha ujasusi cha Ufaransa kimeanzisha uchunguzi wa kina kubaini kilichosababisha tishio hilo.
Post a Comment: