Tunakaribia kuikomboa Ramadi:Iraq
Majeshi ya Iraq
yamesema kuwa yanakaribia kuukomboa mji wa Ramadi baada ya kuanzisha
mashambulizi makali dhidi ya wapiganaji hao wa IS waliokuwa wakishikilia
mji huo tangu mwezi mei mwaka huu.
Maafisa wa vikosi vya serikali
ya Iraq wanasema kuwa hadi sasa wamefanikiwa kuzikomboa wilaya kadhaa
mahala ambapo mamia ya wanadhaniwa kuwepo.
Balozi wa Iraq nchini
Marekani Lukman Faily ameiambia BBC majeshi ya serikali na washirika
wake walikuwa katika hatua za mwisho za kushinda vita hivyo vya
kuukomboa mji huo.
Hata hivyo msemaji wa jeshi la Marekani Colonel
Steve Warren amekaririwa akisema kuwa bado kuna kazi kubwa katika
mapigano hayo dhidi ya kundi hilo la kigaidi.
Post a Comment: