RAIA WANNE WA CHINA WAHUKUMIWA MIAKA 20 JELA
Watuhumiwa wakifikishwa mahakamani .
|
Pembe za Faru walizo kamatwa nazo watuhumiwa hao wanne rai wa China katika Mpaka wa Kasumulu Kyela.
|
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.Jamiimojablog
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mbeya imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela
raia wanne wa China na kulipa faini baada ya kukutwa na hatia kwa
makosa matatu ikiwemo uhujumu uchumi kwa kukutwa na pembe za faru.
Kabla
ya kuanza kusoma hukumu Hakimu mfawidhi Michael Mteite alianza
kuwashukuru Mawakili wa Serikali na Utetezi pamoja na Mkalimani Manfred
Lyoto kwa ushirikiano waliompatia na kuimaliza mapema kesi hiyo kwa siku
23 tu ambapo ameweka historia yeye akiwa Hakimu Mfawidhi kwa kuimaliza
kesi kwa muda mfupi.
Hukumu
hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael
Mteite aliyeanza majira ya saa tano asubuhi na kuahirishwa mara mbili na
kukamilika saa tisa na nusu alasiri ambapo alisema mahakama imeridhika
pasipo shaka kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa
mashtaka katika makosa yaliyokuwa yakiwakabili watuhumiwa hao.
Mteite
alisema Mahakama ilijikita katika kiini cha makosa yote matatu ambayo
ni kupanga kutenda kosa kinyume cha sheria la uhujumu uchumi, kufanya
shughuli za nyara za serikali kinyume cha sheria ya utunzaji ya wanyama
pori inayosomwa pamoja na sheria ya uhujumu uchumi ambapo watuhumiwa
waliingiza pembe 11 za Faru bila kibali.
Alisema
kosa la tatu ni kupatikana na nyara za serikali kinyume cha sheria
chini ya sheria ya uhifadhi ya wanyamapori inayosomwa pamoja na sheria
ya uhujumu uchumi ambapo maeklezo ya washtakiwa walikamatwa wakiwa
wanamiliki nyara za serikali bila kibali cha Mkurugenzi wa wanyama pori.
Hakimu
Mkazi aliendelea kusema ingawa Washtakiwa weote kwa pamoja walikana
mashtaka lakini ushahidi upande wa Jamhuri uliuokuwa na mashahidi tisa
wate walieleza namna watuhumiwa walivyohusika na kosa hilo.
Alisema
uchambuzi wa awali uliofanywa na Mahakama washtakiwa walikubali kwamba
wamesimama mahakamani wakikabiliwa kwa makosa matatu, washtakiwa wa
pili, tatu na nne walikubali kukamatwa Kyela mjini na kurudishwa
mpakani.
Kwa
upande wake mwendesha mashtaka wa Seriakali Wankyo Simon akisaidiwa na
Archiles Mulisa walisema Washtakiwa hawana kumbukumbu ya makosa ya nyuma
ingawa makaso yao yanaonekana yalikuwa yakitendwa kwa kasi kubwa na
wanyama pori wamekuwa wakiathiriwa kiasi kwamba vizazi vijavyo vitakosa
kuona hazina ya wanyama kwa kuwa watakuwav wametoweka.
Alisema
washtakiwa ni raia wa kigeni lakini walikuja nchini kwa lengo la
kufanya utalii katika Mlima Kilimanjaro lakini kumbe nyuma ya pazia kuna
jambo walikuwa wamelipanga hivy Mahakama inapaswa kutoa adhabu kali ili
iwe onyo kwa wengine wenye nia ya kufanya uovu kama huo.
Alisema
Mahakama inapotoa adhabu izingatie kifungu cha 86,1,2 C (ii) cha sheria
ya Uhifadhi ya wanyama pori na kwenye kosa la tatu izingatie kifungu
cha 5 cha mwaka 2009 na kosa la kwanza kla uhujumu uchumi izingatie sura
ya 200 kwani wamevunja mkataba wa kimataifa wa kutunza wanyama walioko
hatarini kutoweka.
Alisema
Mahakama pia izingatie kifungu cha 85 1(b) na (h) ya sheria ya uhifadhi
wanyama pori kwamba nyara zilizokamatwa zinakuwa mali ya serikali ya
Jamhuri ya muungano wa Tanzania sambamba na vifungu vya 111, 1(a), (e)
kwamba chombo kilichotumika kinataifishwa na kuwa mali ya Serikali sawa
na kifungu cha 111(4).
Pia
Wankyo Simon ameiomba Serikali kupitia Mahakama kuwapa tuzo watumishi
wa umma waliowezesha kupatikana kwa nyara hizo na kuokoa raslimali za
Taifa wakiwemo Maafisa Forodha na Askari wa Jeshi la Polisi.
Aidha
Mteite ameiambia Mahakama kuwa Gari namba T 103 DER mali ya Mtuhumiwa
wa kwanza Song Lei likabidhiwa Serikalini na simu za watuhumiwa zitauzwa
na Mahakama hiyo na nyaraka nyingine zitakabidhiwa kwa upande wa
Mashitaka.
Awali
Wakili wa Utetezi Ladislaus Rwekaza aliiomba mahakama kuwapunguzia
adhabu washtakiwa kwa kuwa ni mara yao ya kwanza kutenda kosa, pia ni
raia wa kigeni pia ni vijana wadogo ambao ni nguvu kazi inayotegemewa na
taifa lolote.
Hakimu
Mteite alisema katika hukumu yake amezingatia maombi ya pande zote zote
mbili na kwamba hakuna ubishi kuwa wanyama wanauawa na kuisababishia
serikali inaingia gharama kubwa kuhifadhi wanyama pori ili kunusurui
wanyama kutoweka.
Alisema
katika kosa la kwanza la uhujumu uchumi washtakiwa wanahukumiwa kifungo
jela miaka 15 kila mmoja, kosa la pili kwa mujibu wa kifungo cha
83,84(1) washtakiwa wataenda jela kila mmoja miaka 3 na faini ambayo ni
gharama ya mara mbili ya mali waliokutwa nao hivyo watapaswa kulipa
Dola za kimarekani 836000.
Alisema
katika kosa la tatu kifungu cha 86, 2( c ) inawataka washtakiwa
kutumikia kifungo cha kuanzia miaka 20 hadi 30 lakini Mahakama
inawahukumu miaka 20 jela na kulipa faini ya fedha ambayo ni mara kumi
ya mali waliokutwa nayo ambapo watalipa dola za kimarekani 4180000.
Alihitimisha
kwa kusema Washtakiwa kila mmoja atatumia adhabu zote kwa pomoja ambayo
ni miaka 20 samba mba na faini zilizoorodheshwa.
Alisema watuhumiwa wanahaki ya kukata rufaa kama wataona wameonewa katika hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo.
Washtakiwa
waliohukumiwa kifungo cha miaka ishirini ni pamoja na Song Lei, Xiao
Shaodan, Chen Jinlian na Hu Liang ambao walikamatwa Novemba 6, mwaka huu
mpakani Kasumulu Wilaya ya Kyela mkoani hapa wakitokea nchi jirani ya
Malawi.
Post a Comment: