Mazungumzo ya kutafuta amani Burundi yaanza
Mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa Burundi yameanza rasmi
Jumatatu mjini Kampala Uganda chini ya usimamizi wa mpatanishi rais wa
nchi hiyo Yoweri Museveni.
Waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na wawakilishi wa serikali ya
Burundi, wapinzani wa utawala wa rais Pierre Nkurunzinza , wawakilishi
wa jamii za kiraia na wawakilishi kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Kikao cha Jumatatu kilikuwa ni uzinduzi wa jitihada mpya za kuanzisha na kusukuma mazungumzo ya amani kati ya warundi na majirani zao na hasa jumuiya ya Afrika Mashariki. Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga akihojiwa na Sauti ya Amerika amesema kwamba waliona kuna umuhimu wa kuwasaidia na kuwahimiza kuanzisha utaratibu wa kuzungumza baina yao
Post a Comment: