Mawaziri na Naibu Waziri wapya Kuapishwa Jumatatu 28 Desemba 2015
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
|
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA
BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
Tarehe
23 Desemba, 2015 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli aliwateua Mawaziri wanne, Naibu Waziri mmoja na kumhamisha Wizara
Waziri mmoja.
Walioteuliwa
ni Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge,
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dkt. Joyce Ndalichako na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Hamad Yusuf Masauni.
Rais
Magufuli pia alifanya uhamisho wa Waziri mmoja ambaye ni Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano.
Kufuatia uteuzi huu,
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue anawaarifu Mawaziri wote na Naibu
Waziri walioteuliwa kuwa wataapishwa Jumatatu tarehe 28 Desemba, 2015 Saa tatu asubuhi, Ikulu
Jijini Dar es salaam.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
24
Desemba, 2015
Post a Comment: