Ukawa waeleza sababu za wao kuzomea Bungeni jana
Wabunge wa Ukawa wakitoka bungeni hapo jana.
WABUNGE
wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wameelezea sababu
zilizowafanya wao kuuchukua uamuzi wa kupiga kelele ndani ya bunge kuwa ni
baada ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kuingia Bungeni hali
iliyopelekea kutolewa nje ya Bunge hilo.
Mbunge
wa jimbo la Hai kwa tiketi ya Chadema ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa,
Freeman Mbowe alieleza kuwa, walishindwa kuvumilia kuona ujio wa Dk. Shein
akiingia Bungeni hapo pamoja na Mh. Pandu Kificho ambaye alidai hivi sasa sio
Spika wa Baraza la Wawakilishi kwa kuwa Baraza hilo lilikwisha vunjwa.
Tumeshangaa
kuona Pandu Kificho anaingia kama Spika wa Baraza la Wawakilishi wakati Baraza
limeshavunjwa, tulishangaa kuona Dk. Shein anaingia kama Rais wa Zanzibar
wakati huo kipindi chake cha kukaa madarakani miaka mitano kimekwisha kikatiba,
alisema Mbowe.
Naye
mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alisisitiza kuwa wataendelea
kuonesha msimamo wao huku akimlalamikia Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kuwa
anaendesha Bunge hilo kibabe.
“Leo
hii askari wenye uniform, mae-FFU askari wa fujo wameingia ndani ya ukumbi wa
Bunge. Sasa kwa wasiofahamu, ukumbi wa Bunge katika nchi kama za kwetu na nchi
zinazofuata utaratibu kama wa kwetu, Ukumbi wa Bunge huwa haingii mtu yoyote
asiyekuwa Mbunge. Ndio maana ili Makamu wa Rais na wale wakubwawakubwa
tuliokuwa tunawapigia kelele? waingie, ilibidi tutengue kanuni ili kuwaruhusu
waingie”, alisema Tundu Lissu.
Mwenyekiti
wa Wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), Juma Hamad Omary alimtaja Maalim Seif
Sharif Hamad kuwa kiongozi anayepaswa kuigwa kwa kuwa aliwahi kukubali
kushindwa mara kadhaa licha ya mapungufu kuonekana na kwamba hata alipokuwa
Makamu wa Kwanza wa rais na kisha wawakilishi wa CCM kukataa asuhudhurie kwenye
sherehe za kufunga Baraza la Wawakilishi, aliamua kutohudhuria.
Post a Comment: