SHEIN NA MAALIM SEIF WAKUTANA KUJADILI MUSTAKABALI WA ZANZIBAR
Mazungumzo
ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa visiwani Zanzibar yameendelea huku mkutano
uliowaleta pamoja rais Ali Mohammed Shein na kiongozi wa upinzani Seif Sharif
Hamad ukifanyika.
Kulingana
na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, mkutano huo wa faragha katika ikulu
ya rais ulihudhuriwa na marais wa zamani Ali Hassan Mwinyi na Amani Abeid
karume.
Ni
mara ya kwanza kwa Dkt Shein ambaye anatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Bw
Seif wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye ni makamu wa rais wa kisiwa hicho
kukutana tangu tume ya uchaguzi kufutilia mbali matokeo ya urais.
Kushirikishwa
kwa marais hao wa zamani ni thibitisho kwamba kuna harakati za kisiasa
zinazoendelea katika juhudi za kukabiliana na tatizo hilo ambalo limezua
mgogoro wa kikatiba.
Wanachama
wa jumuiya ya kimataifa pia wanadaiwa kushiriki katika kumaliza tatizo hilo.
Hakuna
habari zilizotolewa kutoka pande zote mbili lakini duru za serikali
zimethibitisha kwamba mazungumzo hayo yalifanyika kwa faragha.
Makamu
wa rais wa pili Seif Ali Idd pia amedaiwa kuhudhuria mkutano huo kulingana na
duru hizo.
Bw
Mwinyi alikuwa rais wa Zanzibar kwa kipindi kifupi cha mwaka 1984 kabla ya kuteuliwa kuwania
urais wa jamhuri ya muungano mwaka 1985 huku Karume akiliongoza eneo hilo kutoka mwaka 2000 hadi mwaka
2010.
Maafisa
wa ikulu ya rais visiwani Zanzibar hawakuwa tayari kuzungumzia kuhusu
yalioafikiwa katika mkutano huo.
Wale
kutoka CUF hata hivyo wamesema kuwa majadiliano yalikuwa mazuri kwa maslahi ya
raia wa muungano wa Tanzania.
Post a Comment: