serikali yachunguza uraia wa Mr bashir ambaye ni Msaidizi wa Lowassa
Maafisa wa polisi nchini
Tanzania wamesema kuwa wanamzuia msaidizi wa aliyekuwa waziri mkuu wa taifa
hilo Edward Lowassa ili kuchunguzwa kuhusiana na uraia wake.
Kulingana na gazeti la The
Citizen nchini humo,wamesema kuwa bwana Bashir Fenel Awale Ally ambaye amekuwa
mtu muhimu katika kampeni za urais za bwana Lowassa atachunguzwa kuhusiana na
stakhabadhi zinazotilia shaka kuhusu uraia wake.
Kamanda maalum wa polisi
katika eneo la Dar es Salaam, Suleiman Kova amewaambia waandishi wa habari
kwamba stakhabadhi alizokamatwa nazo zinatatiza kuhusiana na taifa analotoka.
Amesema kuwa wakati wa
kukamatwa kwake mtu huyo alipatikana na cheti cha kuzaliwa kinachoonyesha kwamba
alizaliwa tarehe 11 mwezi Julai mwaka 1969 mjini Dodoma.
Kulingana na afisa huyo
mshukiwa huyo pia alipatikana na pasipoti iliotoka jijini nairobi na ambayo
inayoonyesha kwamba alizaliwa mjini humo mnamo tarehe 11 mwezi Julai mwaka
1969,akiwa na jina la Bashir Fenal Abdi Ally Awadhi .
Mshukiwa huyo anayedaiwa
kuwa mwanaharakati na mfuasi mkubwa wa chama cha upinzani Chadema alikamatwa
nyumbani kwake huko Mikocheni.
Kova amesema kuwa kuna
ishara kwamba mshukiwa huyo ni raia wa Kenya.
Ameongezea kuwa sheria za
Tanzania haziruhusu mtu asiye raia wa taifa hilo kushiriki katika maswala ya
kisiasa ikiwemo kushiriki katika kampeni na kupiga kura.
Post a Comment: