MAGUFULI AFUTA SAFARI ZA WATUMISHI WA SERIKALI NJE YA NCHI

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli jana asubuhi katika
Ikulu ya Dar es Salaam amefanya kikao na Makatibu wakuu, Manaibu Makatibu
wakuu, Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) ili kutoa uelekeo wa Serikali anayoitaka mara baada ya
kuapishwa.
“Nataka
Serikali iendelee kwa nguvu zote na katika kutekeleza dhana ya ‘HAPA KAZI TU’
na viongozi kuzingatia na kukumbuka ahadi nilizotoa ili zianze kuonekana na
kufanyiwa kazi mara moja” Rais Magufuli amesema.
Katika
Kikao chake, Rais ametoa mwongozo na kusisitizia kuwa ni lazima kila mtendaji
Serikalini kuuzingatia, kufuata sheria na taratibu ili taifa lisonge mbele kwa
ufanisi zaidi.
Katika
kikao hicho Rais ameelekeza mambo kadhaa ambayo watendaji hao wanapaswa
kuyasimamia, kuyawekea mikakati na kuyapanga vizuri ili atakapo teua Baraza
lake la Mawaziri mambo hayo yawe tayari ili Mawaziri watakaoteuliwa waweze
kuyasimamia bila kukosa.
Mambo
hayo muhimu ni kama ifuatavyo:
Kuanzia
mwezi Januari mwaka 2016, wanafunzi wote wanaoanza shule watasoma bure bila
kulipa ada, Katika jambo hili, Rais amewataka watendaji kuanza kuliwekea mikakati
tayari kwa utekelezaji
Suala
la mikopo ya wanafunzi nalo lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike kwa ajili
ya utekelezaji mzuri zaidi.
Amefuta
safari zote za nje ya nchi kuanzia leo hadi hapo atakapolitolea suala hilo
maamuzi mengine na kueleza kuwa shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchi
zifanywe na kusimamiwa na mabalozi wa Tanzania wanaowakilisha nchi huko nje.
Pengine
patokee jambo la dharura sana na hata hilo lazima kibali kitolewe na Rais au
Katibu Mkuu Kiongozi. Badala yake Rais amewataka watendaji hao kufanya zaidi
ziara za kwenda vijijini ili kuzijua na kutatua kero za wananchi wa Tanzania.
Katika
Kikao hicho, Rais amemtaka Kamishna wa TRA, Ndugu Rished Bade kusimamia kwa
makini zoezi la ukusanyaji wa mapato nchini na kuhakikisha kero ndogo ndogo kwa
wananchi lianze kutekelezwa kama alivyo ahidi kwa kufanyiwa kazi mapema zaidi.
Rais
ameitaka TRA kukusanya mapato hayo kutoka kwa wafanya biashara wakubwa zaidi na
wale wanaokwepa kodi bila kuogopa mtu wala taasisi yoyote hapa Tanzania na
kusisitiza kuwa katika Serikali hii wa kutoa maamuzi vinginevyo zaidi ya haya
ni yeye Rais ama Makamu wake.
Rais
Magufuli pia ameagiza usimamizi katika suala la manunuzi ambalo limekuwa
likitumika vibaya na kuwa mwanya wa kuibia Serikali kwa watu kuongeza bei ya
vitu hata kama ni vya bei ndogo kabisa katika jamii.
“Ikitokea
suala hilo likagundulika kwa watu kuongeza bei ya vitu, watendaji
watawajibishwa mara moja”. Rais amesema, na kuwataka watendaji hao kufanya kazi
zao kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo na kuzingatia maadili mema ya
kazi.
………………………MWISHO……………………
Imetolewa
na Premi Kibanga,
Mwandishi
wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
Post a Comment: