PANGA LA MAGUFULI LAHAMIA TACAIDS,AZUIA SIKU YA UKIMWI DUNIANI
Rais John Magufuli
amesitisha maadhimisho ya siku ya Ukimwi
kitaifa ambayo yalikuwa yafunguliwe mkoani Singida leo na kufikia kilele chake
Desemba mosi mwaka huu mjini humo.
Badala yake Rais Dk Magufuli
ameagiza fedha zote ambazo zilitengwa na serikali pamoja na wahisani mbalimbali
kwaajili ya maadhimisho hayo zielekezwe kununua dawa kwaajili ya waathirika wa
Ukimwi na vitendanishi.
Akizungumza na moja kwa moja
na Televisheni ya Taifa (TBC), Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya
Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk Fatma Mrisho, alisema serikali imeagiza jana
wakati tayari mkuu wa Mkoa wa Singida akiwa ameshafungua maonesho ya
maadhimisho hayo.
“Serikali imesitisha
maadhimisho ya mwaka huu Singida na badalayake fedha zilizopangwa kwaajili ya
maadhimisho ziende zikanunue dawa za virusi vya Ukimwi, dawa za kudhibiti
maambukizi ya ukimwi na vitenganishi,” alisema Mrisho.
Dk Mrisho alisema kuwa
tayari taarifa za kusitisha maadhimisho hayo zimesha wafikia washiriki na wale
walio kuwa njia kuelekea Singida wamegeuza.
SOMA ZAIDI BOFYA HAPA.
Katika maadhimisho ya mwaka
huu serikali ilitenga kiasi cha shilingi
Milioni 18 kwaajili ya maadhimisho hayo huku kila mshiriki katika maonesho
hayo akiachangia kiasi cha sh laki tano.
Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa
ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk Fatma Mrisho alisema maadhimisho ya mwaka huu
yakuwa yatanguliwe na maonesho ya wadau yatakayojumuisha huduma mbalimbali
zikiwamo za utoaji elimu na burudani.
Dk Mrisho alisema huduma
nyingine zilizopangwa kutolewa katika maadhimisho hayo ya wiki moja ni upimaji
wa hiari wa watu zaidi ya 3,500
wanaoishi na virusi vya Ukimwi na utoaji ushauri nasaha, upimaji wa
shingo ya uzazi, sukari, uzito, damu na kupata elimu itakayotolewa kupitia
vikundi vya sanaa na burudani.
Maadhimisho ya mwaka huu
yanachagizwa na kaulimbiu ya ‘Tanzania bila maambukizi mapya ya VVU, vifo
vitokanavyo na Ukimwi na ubaguzi na unyanyapaa inazewekana.’
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk
Parseko Kone aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni kuwa
maadhimisho hayo yanatarajiwa kuanza Novemba 24 mwaka huu kwenye viwanja vya
Peoples Club ambapo uzinduzi utakuwa Novemba 25 kabla ya kilele, Desemba mosi.
Hii ni mara ya tatu tangu
Rais Dk Magufuli aingie madarakani kuzuia maadhimisho yanayogharimu fedha
nyingi na sherehe na fedha zake kuelekeza ikanunulie vifaa tiba mahospitalini.
Awali Rais aliagiza fedha
zilizotengwa kwaajili ya hafla ya uzinduzi wa Bunge zaidi ya shilingi Milioni
225 ziende kununulia vitanda vya hospitali ya taifa Muhimbili.
Aidha Rais pia alisitisha
maadhimisho ya siku ya Uhuru Desemba tisa mwaka huu na badala yake watu wafanye
kazi katika maeneo yao ya kazi hasa usafi wa mazingira.

Post a Comment: