MWAKALEBELA AENDA MAHAKAMANI KUMPINGA MCH MSIGWA
Aliyekuwa
mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Frederick Mwakalebela amefungua kesi ya
kupinga matokeo ya uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Iringa mjini yaliyompa
ushindi Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema huku akiitaja kofia ya M4C katika
shtaka lake.
Msajili
msaidizi wa mahakama kuu ya kanda ya Iringa , Ruth Massama amesema kuwa
Mwakalebela alifungua shtaka hilo mahakamani hapo Oktoba 30 mwaka huu.
Katika
shitaka hilo, pamoja na mambo mengine, Mwakalebela anamtuhumu Msigwa kwa
kuvunja sheria ya uchaguzi kwa kuvaa kofia yenye nembo ya M4C inayotumiwa na
Chadema, katika siku ya kupiga kura.
Kadhalika,
mlalamikaji huyo anamtuhumu mwangalizi wa uchaguzi kwa kukiuka sheria na kanuni
za uchaguzi wakati wa zoezi la kupiga na kuhesabu kura.
Katika
madai yake, Mwakalebela ameeleza kuwa katika kata ya DaboDabo alikataliwa
kuingia katika kituo cha kupigia kura wakati wakati mshindani wake huyo
aliruhusiwa kuingia bila kizuizi chochote.
Msimamizi
wa uchaguzi katika jimbo la Iringa Mjini alimtangaza Mchungaji Peter Msigwa
kuwa mshindi wa nafasi hiyo hivyo kupata nafasi ya kuendelea kuliwakilisha
jimbo hilo kwa muhula wa pili.
Post a Comment: