MAGUFULU ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA UFARANSA NCHINI
Rais
Dk John Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo katika ofisi za Ubalozi wa
Ufaransa nchini kufuatia mauaji ya watu 132 kutoka mataifa mbalimbali
yaliyofanywa na magaidi katika mji wa Paris, Ufaransa hivi karibuni. Kulia ni
Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak. Rais Magufuli alisaini kitabo hicho Dar es Salaam leo.
Rais
Dk John Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo katika ofisi za Ubalozi wa
Ufaransa nchini kufuatia mauaji ya watu 132 kutoka mataifa mbalimbali
yaliyofanywa na magaidi katika mji wa Paris, Ufaransa hivi karibuni.
Rais
Dk
John Magufuli akimkabidhi Balozi Ufaransa nchini, Malika Berak barua
ya salamu za maombolezo bakitia baada ya kusaini kitabu cha maombolezo
katika ofisi za Ubalozi wa
Ufaransa nchini kufuatia mauaji ya watu 132 kutoka mataifa mbalimbali
yaliyofanywa na magaidi katika mji wa Paris, Ufaransa hivi karibuni.
Rais
Dk John Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufarasa nchini, Malika Berak na kumpa pole.
Rais Magufuli akiwa na watumishi wa ubalozi huo
Rais Dk Magufuli akiagana na Balozi wa Ufaransa.
************
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesaini
kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam
kufuatia vifo vya watu zaidi 130 vilivyotokea November 15, 2015 kutokana
na mashambulizi ya ugaidi mjini Paris, Ufaransa.
Pamoja na
kutia saini kitabu cha maombolezo, Mheshimiwa Dr. Magufuli ametoa
salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande na
kumuombea uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu.
Dk.Magufuli
ambaye amepokelewa na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bibi Malika Berak
amesema Tanzania imeguswa na vifo hivyo na inaungana na Ufaransa katika
kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Aidha
Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wa tukio hilo wapone haraka ili
waweze kuungan a na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila
siku.
Katika
hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe
Magufuli amewasili Mjini Dodoma jioni hii kwa shughuli mbalimbali za
kikazi.
Mheshimiwa
Magufuli amesafiri kwa gari kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na taarifa
ya shughuli atakazozifanya mtaarifiwa baadaye.
Post a Comment: