Lowassa ataka ahadi za Dk. Magufuli zipimwe
ALIYEKUWA
Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa,
amewataka wananchi kulinganisha ahadi za Rais, Dk. John Magufuli na
CCM kuhusu elimu.
Ameyasema
hayo siku mbili baada ya Dk. Magufuli,
aagize watendaji wa serikali kushughulikia utekelezaji wa sera yake ya kutoa
elimu bure kuanzia Januari mwakani.
Lowassa,
chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), aliahidi kutoa elimu
bure kuanzia shule ya awali hadi chuo kikuu.
Pia
alikuwa ameahidi kufuta michango
yote wanayotozwa wanafunzi, kama
angepata ushindi wa kuwa rais.
Dk.
Magufuli ambaye alikuwa akipeperusha bendera ya CCM, aliahidi kutoa elimu bure
hadi kidato cha nne.
Taarifa iliyotolewa jana na ofisi binafsi ya
Lowassa, ilisema ahadi ya elimu bure aliyokuwa akiinadi, ilikuwa iwaguse hata
wanafunzi ambao tayari wako shuleni na siyo wanaotarajiwa kuanza mwakani pekee.
“Niliahidi
watoto wote walioko na watakaoanza shule kuanzia kindergarten (shule ya awali)
hadi chuo Kikuu serikali yetu ingegharimia.
“Na
nilitangaza kufuta michango yote shuleni
kumpunguzia mzigo mwananchi,” taarifa hiyo ilimnukuu Lowassa akisema.
Taarifa
hiyo ilisema ahadi ya Dk.
Magufuli, “ni kwamba kuanzia Januari
hakuna mtoto atakayelipa ada lakini hajatamka mustakhabali wa wanafuzi walioko
shuleni kama wataguswa na hatua hiyo au laa.”
Kuhusu
mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, taarifa hiyo ilisema, Chadema kupitia
Lowassa kilikwisha kuahidi kuwa elimu ingekuwa bure hadi chuo kikuu.
“Vijana
hawa wanahangaika na mikopo nasikia ni asilimia 17 tu kati ya wanafunzi 70,000
ndiyo waliopata mikopo.
CHANZO :http://mtanzania.co.tz/?p=7489
Post a Comment: