HEKAHEKA ZA BARAZA LA MAWAZIRI

Siku chache baada ya kufuta safari za vigogo nje ya nchi,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli anakusudia kufyeka wizara 8 miongoni mwa 28 zilizopo sasa ili kubana matumizi.
Hatua hiyo
ya Dr Magufuli
ni sehemu ya
utekelezaji wa ahadi
alizozitoa kwa wananchi
wakati akijinadi kwenye
kampeni zake za
kuwania Urais kupitia
Chama cha Mapinduzi-CCM
kwamba atapunguza ukubwa
wa serikali kwa
kuunda baraza dogo
la mawaziri.
Katika miaka 10
ya uongozi wa
Rais Kikwete, kumekuwa na
malalamiko ya ukubwa
wa baraza la
Mawaziri huku baadhi
ya wizara zikiwa
na mawaziri watatu.
Kwa mkakati
huo,endapo Dr Magufuli
ataweza kufyeka Wizara 8,
maana yake atakuwa
amewatupa nje ya
ajira vigogo zaidi
ya 20 ambao ni
mawaziri na manaibu
wao pamoja na
makatibu wakuu na
manaibu wao ambao
kasma zao za
mishahara ni mzigo
mkubwa kwa serikali
Baraza la
kwanza la Rais
mstaafu Kikwete mwaka 2005
lilikuwa na Mawaziri
na Manaibu wao 60, jambo
ambalo lililalamikiwa na
wadau wengi kwamba
halina tija bali
lilikuwa na lengo
la kulipana fadhila
Taarifa zaidi
zinasema kuwa huenda
Rais Magufuli akachelewa uteuzi wa
mawaziri hadi Disemba
mwaka huu ili
kujipa muda zaidi
wa kuangalia na
kufanya uchambuzi wa
wizara zipi za
kuzifyeka kwani baadhi
hazina tija
Wizara
zilizo Hatarini Kufyekwa
Ingawa
Rais Magufuli hajazitaja
Wizara zitakazofyekwa,
lakini habari toka
serikalini zinasema kuna uwezekano
mkubwa wizara zisizo
na tija na zinazoweza
kuunganishwa na kuwa
idara chini ya
wizara fulani, zikafyekwa.
Wizara hizo
ni Maendeleo ya
Jamii,Jinsia na Watoto
ambayo huenda ikaingizwa
kwenye ofisi ya
Makamu wa Rais, hasa
wakati huu ambapo
ofisi hiyo inashikiliwa
na mwanamke.
Nyingine ni
wizara iliyokuwa ikishughulika
na mambo ya
utawala bora ambayo
wadadisi wa masuala
ya siasa wanapendekeza
iwe chini ya Wizara ya
mambo ya ndani
pamoja na Takukuru
ili kukabiliana na
Rushwa.
Wizara ya
Nchi,Ofisi ya Makamu
wa Rais Mazingira
nayo inaweza kufyekwa
na suala la
Mazingira likasimamiwa na
kila Wizara kwa
kuwa na kitengo
chake cha kusimamia
mazingira badala ya
kuwa na Waziri
wake.
Wizara ya
uwekezaji na uwezeshaji
huenda ikafutwa na
kuingizwa ndani ya
kituo cha uwekezaji ( TIC ) na
kuwa idara nyeti
ya kusimamia maswala
ya uwekezaji ikiwa
chini ya wizara
ya Viwanda na
Biashara.
Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo
nayo inapumulia mashine
kwani huenda ikaungana
na Idara ya
Habari (Maelezo) na kuwa
idara zilizo chini ya
ofisi ya Waziri
mkuu badala ya
kuwa Wizara kamili
Wizara ya
Kilimo na Mifugo
inapendekezwa kuwa moja
badala ya mbili
kama ilivyosasa.Waziri katika
ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) iliyokuwa
inashikiliwa na Profesa
Mwandosya yenyewe imekufa
kifo cha Mende,kwani
hakuna ubishi kwamba
itafyekwa.
Post a Comment: