Hatimaye Magufuli aanza kazi rasmi kwa kumteua mwanasheria mkuu wa serikali
Dar es Salaam. Saa chache baada ya kuapishwa kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano, Dk John Magufuli jana amemteua George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es
Salaam Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni
Sefue amesema Rais Magufuli atamwapisha mwanasheria Masaju kesho asubuhi ili
kuanza majukumu yake mara moja kwa mujibu wa sheria.
Aidha Balozi Sefue amesema kuwa, Rais
Magufuli ameitisha rasmi kikao cha kwanza cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kitakachoketi Novemba 17, mwaka huu.
Katibu Mkuu kiongozi amesema Rais
Magufuli atarajiwa kupendekeza jina la Waziri Mkuu ambalo litawasilishwa katika
bunge hilo jipya Novemba 19 ili lipigiwe kura.
Post a Comment: