BAADA YA ZIARA YA GHAFLA MUHIMBILI : MH DKT MAGUFULI AVUNJA BODI YA UONGOZI MUHIMBILI ATEUA UONGOZI MPYA-OMBENI SEFUE
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana
amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana
na hali ya kumsikitisha.
“
Rais amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan
wanaolala chini. Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia
vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa
kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa,
ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na
wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko”.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema na kutoa maelekezo yafuatayo :
Rais
amevunja Bodi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ilishamaliza muda wake
na amemteua Prof. Lawrence Mseru , kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa
Muhimbili kuanzia kesho tarehe 10 Novemba, 2015.
Dkt.
Hussein L. Kidanto ambaye ndiye anayekaimu hivi sasa, amehamishiwa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii ambako atapangiwa kazi nyingine.Balozi Sefue pia
amesema, Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi ya wiki mbili kwa
uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine zote za uchunguzi wa magonjwa
ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na kuhudumia wananchi kama ipasavyo.Tayari
Wizara ya Fedha imetoa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kazi hiyo na kulipa
madeni ya ukarabati wa mashine za uchunguzi wa magonjwa nchini.
Hata
hivyo Katibu Mkuu Kiongozi amesema kuanzia sasa hospitali zote nchini
zinatakiwa kutenga fedha kutoka kwenye mapato yao wenyewe na kuhakikisha
mashine na vifaa vyote vya kazi vinafanya kazi wakati wote (Regular
Maintenance).
Balozi
Sefue pia metumia nafasi hii kuwaagiza watendaji na viongozi wote katika sehemu
za kazi kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo na kazi za umma
zinatekelezwa ipasavyo.
“Hakutakuwa
na huruma kwa watumishi wa Umma wasiojali wananchi na mahitaji yao” Amesisitiza
Balozi Sefue.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari
wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es
Salaam.
9 Novemba, 2015
Post a Comment: