WENJE ANGURUMA MWANZA
MGOMBEA Ubunge wa jimbo la Nyamagana, Ezekia Wenje (Chadema), amesema
Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imechangia kuiuwa elimu na
imeshindwa kutafuta mbinu na mikakati ya kuikomboa isiangamie.
Kauli hiyo aliitoa juzi wakati wa mkutano wa hadhara, uliofanyika katika viwanja vya Bendera Tatu, Kata ya Bugarika, Nyamagana jijini hapa na kuhudhuliwa na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara, Vicent Nyerere.
Wenje ambaye pia ni Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani, amesema kuwa
kitendo cha serikali ya CCM kuendelea kushusha madaraja ya ufaulu
kuanzia elimu ya msingi na sekondari imesababisha Taifa kuendelea
kushuka kielimu.
Amesema kuwa CCM wanafanya kitendo hicho kwa manufaa yao binafsi na
kuamini ndiyo itakuwa msaada katika safari yao ya kisiasa ili
kuwaaminisha watanzania elimu inayotolewa ni bora kumbe ni chanzo cha
kuongeza ujinga kwa watoto wa masikini.
Hata hivyo amesema watanzania wanapaswa kuwapa kura za ndiyo wagombea
wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akiwamo, Edward Lowassa ili
kuboresha mitaara ya elimu nchini, na kuondoa ada za shule kuanzia
`vidudu` hadi chuo kikuu.
Mgombea ubunge Jimbo la Musoma Mjini, Vicent Nyerere (Chadema)
amewataka watanzania kupuuza propaganda za CCM za kuwadanya kuwa,
mgombea Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa ni mgonjwa kwani sio
sehemu ya wabeba vyuma na watunisha misuri.
“Kazi ya hao wenzetu CCM ni uongo na aibu ya kushindwa uchaguzi huu
ndo inayowasumbua na sasa wamekosa hoja wameanza kuongea bila mpangilio
na kuwaeleza watanzania watawafanyia nini kazi yao ni kuwapuuza,”
amesema Nyerere.
Nyerere ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara, amesema ni
wakati wa mabadiliko kwa kuwa watanzania walishachoka na ahadi za uongo
zisizotekelezeka na kusababisha watanzania kuendelea kuishi maisha ya
duni.
Mmoja wa wananchi waliohudhulia mkutano huo, Edward Madale, amesema
kutokana na CCM kushindwa kuwatekelezea na kutatua kero zao umefika
wakati muafaka wa kuacha kukichagua.
Post a Comment: