WARAKA WA MH EDWARD LOWASSA KWA WATANZANIA
Ndugu waandishi wa habari;
Tumewaita
hapa kuwaomba muwaeleze Watanzania wenzetu, jumuiya ya kimataifa na marafiki
zetu wengine wa ndani na nje, kwamba hatukubaliani na matokeo ya uchaguzi mkuu
wa rais, yanayoendelea wa mkono na UKAWA, Maalim Seif Sharif Hamad.
EDWARD
LOWASSA
MGOMBEA
URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAkutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), kote nchini.
Hii
ni kwa sababu, upo ushahidi wa wazi unaothibitisha kwamba utangazaji wa matokeo
hayo umevurugwa kwa makusudi na watendaji ndani ya NEC kwa kusaidiana na Chama
Cha Mapinduzi (CCM).
Katika
maeneo mengi ambako matokeo yameshatangazwa mpaka sasa, kilichoripotiwa kuwa
matokeo ya uchaguzi wa urais, hakifanani wala kuendana na matakwa halisi ya
wananchi.
Matokeo
mengi yamesheheni udanganyifu, ulaghai na yameandaliwa kwa lengo maalum la
kumbeba mgombea wa CCM, John Pombe Magufuli.
Katika
baadhi ya majimbo ya uchaguzi, kura zetu zimepunguzwa na kuongezwa kwa mgombea
wa CCM; maeneo mengine, kura zilizotangazwa zimetofautiana na idadi halisi ya
kura zilizopigwa.
Kwa
mfano, matokeo yaliyotangazwa na NEC katika majimbo ya Mkoani na Mtambile,
kisiwani Pemba, Makunduchi, Kiwengwa, Donge, Tunduru, Tunduma, Same Mashariki,
Chambani, Tandahimba, Kilindi na kwingi kwingineko, ni miongoni mwa matokeo
yanayothibitisha kuwa hiki kinachotangazwa na NEC, siyo kura za uchaguzi mkuu
wa rais. Tunaweza kuiita, “mzimu wa uchaguzi.”
Ndugu
waandishi wa habari;
Tangu
kuanza kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi huu, viongozi wetu wanaounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA) – mimi mwenyewe juzi na jana Mhe. Freeman Mbowe,
James Mbatia na Profesa Abdallah safari walilieleza kasoro zilizojitokeza
katika matokeo ya rais,
Hata
hivyo, Tume imeendelea kutangaza matokeo hayo, bila kujali kile ambacho
tumekieleza na kukilalamikia, kana kwamba tunachokisema ni ujinga, uzushi na
uwendawazimu. Hili halikubaliki.
Aidha,
katika maeneo mengine, likiwamo jimbo la Ubungo, matokeo yaliyoko mikononi mwa
msimamizi wa uchaguzi, yanatofautiana na yale ambayo yamekusanywa kutoka katika
vituo vyote vya jimbo hilo.
Hali
kama hiyo ipo pia katika majimbo yote ambayo wagombea wa CHADEMA na wale wa
vyama washirika vya CUF na NCCR – Mageuzi, ama wamekuwa na nguvu kubwa au
wameibuka washindi.
Upo
ushahidi wa wazi ambao, ninyi waandishi mnaweza kwa kutumia uandishi wenu
kuuthibitisha kwamba, katika majimbo yote ambako wagombea wa UKAWA wameshinda,
TUME imechelea kutangaza matokeo ya urais kwa sababu zinazothibitisha kuwapo
kwa mikakati ya hila.
Ikumbukwe
kwamba matukio yote haya ya NEC kutangaza matokeo yaliyochakachuliwa yamekuja
baada tu ya Jeshi la Polisi kuvamia vituo vyetu vitatu vya kuhesabia kura na
kuwakamata wataalam wetu waliokuwa wakipokea matokeo ya kura za rais nchi nzima
ambayo hadi uvamizi huo ulipofanyika tulikuwa tukiongoza katika maeneo
mbalimbali.
Ndugu
waandishi wa habari;
Tunaamini
kwa dhati kwamba, uvamizi huo ulifanyika mahususi kwa malengo ya kufanikisha
uchakachuaji huo ambao sasa tunauona ukiendelea kufanyika kupitia matangazo
yanayoendelea kutolewa sasa na NEC.
Wakati
tukijua kwamba NEC ndiyo mamlaka pekee ya kisheria ya kutangaza matokeo ya
urais, tunapenda kuwataarifu Watanzania na jumuiya ya kimataifa kwamba hadi
wakati uvamizi huo ulipofanyika kura zetu za urais tulizokuwa tumezikusanya
zilikuwa zikionyesha tukiongoza kwa asilimia zaidi ya 60.
Kutokana
na makosa hayo makubwa na ya makusudi yanayofanywa na watendaji wa NEC, mimi
Edward Ngoyai Lowassa, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano na Mgombea Mwenza,
Juma Duni Haji, tunautangazia umma wa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa,
kwamba hatukubaliani na matokeo yanayotangazwa na NEC.
Ndugu
waandishi wa habari;
Kutokana
na makosa hayo makubwa, tunaitaka NEC kusitisha mara moja utangazaji wa matokeo
ya urais na kuanza upya kufanya uhakiki wa kile wanacholetewa na wasimamizi wa
majimbo ambacho ushahidi unaonyesha kuwapo kwa vitendo vya hila ambavyo
vinafanywa na NEC.
Ndugu
wana habari
Kile
kinachofanywa na NEC hapa ndiyo kile kile kinachoendelea kufanywa kule Zanzibar
leo na ZEC ambako kunafanyika juhudi kubwa na za makusudi kupora kwa hila na
kwa mabavu mwelekeo wa wazi wa ushindi wa Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi
ya CUF anayeungwa mkono na UKAWA, Maalim Seif Sharif Hamad.
EDWARD
LOWASSA
MGOMBEA
URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Post a Comment: