UONGO WA CCM NA STAR TV KATIKA URUSHWAJI LIVE MIKUTANO YA CCM
Ni karibu mwezi mzima CCM imekua ikirusha live mikutano yao ya kampeni za urais na tangu waanze kurusha kupitia chaneli hii iliochini ya sahara media (star tv) sijawahi ona wakionyesha mkutano ambao hawakujaza uwanja (maarufu mafuriko) kiasi nikaaanza kuamini kuwa chama cha mapinduzi bado kinapendwa sana na watanzania.lakini kumbe hawa ndugu zetu wanatumia vibaya maendeleo ya teknolojia na kuwa wadanganya watanzania.
kwa ufupi tizama hii video hapo juu kwa kile kilichoendelea kwenye mkutano wa moshi mjini jana tarehe 7/10/2015 upate kuelewa hali halisi ilivyokua na kile kinachofanywa na media hii ya star tv mali ya mwenyekiti wa ccm mkoa wa mwanza Bw Antony Diallo
Post a Comment: