Uchaguzi wa Handeni mjini waahirishwa rasmi
Uchaguzi wa ubunge
katika jimbo la Handeni mjini nchini Tanzania umeahirishwa kufuatia kifo
cha mgombea wa eneo hilo kupitia tiketi ya chama cha CCM Daktari
Abdallah O Kigoda.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa tume ya Uchaguzi
Kailima Kombwey shughuli za kampeni za uchaguzi tayari zimesitishwa
katika eneo hilo.
Kombwey amesema kuwa tume hiyo itatangaza ratiba ya tarehe ya uteuzi wa mgombea mwengine kutoka chama cha Mapinduzi CCM.
Hatahivyo kampeni nyingine za Urais na Udiwani katika jimbo hilo zitaendelea kama kawaida.
Post a Comment: