TUJIKUMBUSHE TATHMINI YA USHINDI WA UKAWA UCHAGUZI WA JUMAPILI 25/10/2015
IKIWA
zimebaki siku mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu kufanyika, Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) umetoa tathmini yake ya ushindi kwa asilimia 61 kwa wagombea
wake wanaogombania nafasi ya urais, ubunge na udiwani.
Tathmini
hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Ukawa, Regnald Munisi, wakati
akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu uchaguzi huo.
Alisema
tathmini hiyo waliifanya mikoa yote kwa sampuli ya watu 30,000.
“Tuna
uhakika kwa ushindi wa asilimia 61, na kama ikishuka sana itakuwa asilimia 58,
na ikipanda ni kwa asilimia 64, na mtaona itakavyokuwa katika matokeo, ndivyo itakuwa
hivyo,” alisema Munisi.
Alisema
hawataukubali mfumo wa kuhesabia kura kwa vifaa ambavyo hawana uhakika navyo,
ikiwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itagoma kuwashirikisha ili wajiridhishe
navyo kabla ya kuvitumia kwa kudai kuwa wanawaingilia.
“Kila
chama kinapaswa kuridhika na matumizi na utendaji wa mashine hizo za kuhesabia
kura, hatutaweza kukubali kutumia mashine hizo kama zinaweza kuwa na matatizo,”
alisema Munisi.
Aidha
aliitaka NEC kutoa idadi ya mwisho ya vituo vya kupigia kura ili waweze
kupeleka mawakala wao.
Alisema
NEC imekuwa ikitoa idadi tofauti kwa vipindi tofauti kwa kuwa mwanzoni ilidai
vituo vitakuwa 72,000, baadaye ikatangaza 65,000 na sasa 63,000.
“Wasiwasi
ni kwamba NEC inaweza kutangaza idadi ya vituo vipya, na ikaongezeka wakati huu
wa mwisho, hivyo inawezekana mawakala washindwe kuwepo katika vituo hivyo kama
hatuvijui mapema,” alisema Munisi.
Pia
aliitaka NEC kueleza kama kuna idadi ya watu iliyoongezeka katika daftari la
wapigakura na ilikuwaje wasiwepo awali.
“Watueleze
tujue ni wangapi na kuona kama itawezekana kwa kuwa kama ni wengi kama milioni
moja, hatuwezi kukubali kwa kuwa hatuna uhakika nao, lakini kama ni wachache
kama 100 tunaweza kuelewana baada ya kuongea,” alisema Munisi.
Post a Comment: