TUJIKUMBUSHE : HUYU NDIYE JUMA HAJI DUNI

JUMA HAJI DUNI - MGOMBE MWENZA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUPITIA CHAMA CHADEMA CHINI YA MWAMVULI WA UKAWA
Mwanasiasa
machachari wa upinzani kutoka Zanzibar, Juma Duni Haji mgombea mwenza wa mgombea urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Edward Lowassa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA); aliteuliwa kuwa mgombea mwenza mara tu baada ya mwanasiasa huyo
kukihama Chama cha Wananchi (CUF) ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA - vyama vingine vilivyomo kwenye
Ukawa ni NCCR-Mageuzi na National League for Democracy (NLD)).
Viongozi
wa UKAWAwalipokutana kupitia majina ya wanasiasa wenye sifa ya kuwa wagombea
wenza, walikubaliana kumteua mwanasiasa huyo ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti
wa CUF na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inayofanya
kazi chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
Mwanasiasa
huyo amekuwa na historia ndefu na mara tatu amewahi kuteuliwa na CUF kuwa
mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano, akiwa na Mwenyekiti wa chama
hicho, Profesa Ibrahim Lipumba. Amekuwa mgombea mwenza wa Profesa Lipumba
katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, mwaka 2005 na mwaka 2010. Duni amewahi
kunukuliwa akieleza kuwa yeye ni mtumishi wa watu na kila mara alikotumwa
alikwenda. Hivyo, hata leo akiteuliwa kwenda kuongoza kijiji au kitongoji
ilimradi Watanzania wametaka hivyo, ataitikia wito.
Juma
Duni alianza safari ya kisiasa kwa “kulazimishwa” mwaka 1984, baada ya Serikali
ya Muungano kutoa Waraka wa Serikali (White Paper) na kutakiwa wananchi watoe
maoni yao juu ya hali na matatizo ya Muungano.
Wakati
huo, makatibu wakuu wa Serikali ya Zanzibar akiwamo yeye walitoa maoni dhidi ya
muungano. Uhuru huo wa kitaalamu uligeuzwa kuwa mchungu kwani walisingiziwa
kwamba wamefanya kinyume na walivyoagizwa na baadhi yao wakapewa onyo kali na
wengine wakateremshwa vyeo.
Juma
Duni aliteremshwa cheo kutoka wadhifa wa Katibu Mkuu hadi mwalimu wa kawaida
kwa Tangazo la Rais. Huko nako pia hakubaki salama kwani alituhumiwa kuwajaza
wanafunzi kasumba, hivyo alirudishwa Wizara ya Elimu kama Ofisa Mipango ambako
pia alituhumiwa kujihusisha na siasa za upinzani. Duni alipoona amechoka
kuhamishwahamishwa na kushutumiwa, aliomba likizo ya bila malipo kwenda kusoma,
ombi ambalo pia lilikataliwa.
Hapo
ndipo alipoamua mwenyewe kuondoka na kwenda kujisomesha kwa fedha zake Chuo
Kikuu cha Manchester, Uingereza na kuhitimu stashahada ya Juu ya Biashara kati
ya mwaka 1993-1994. Alipofika Uingereza, akatumiwa barua ya kuachishwa kazi na
kupoteza haki zake zote za miaka 18 ya utumishi serikalini.
Mwaka 1994 akiwa bado
nchini Uingereza, akaunganisha masomo na kusomea
Shahada ya Uzamili akibobea
kwenye usimamizi wa Rasilimali Watu na kabla
hajahitimu akarejea nchini ili
kusaidia upinzani kujipanga kiuchaguzi. Moja
kwa moja akajiunga na vuguvugu la
uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi
akajiunga na CUF na akateuliwa kuwa mgombea
mwenza wa mgombea urais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama
hicho, Profesa
Lipumba wakati bado hajakamilisha shahada yake ya pili ya
uongozi na utawala
Post a Comment: