Sunday, 25 October 2015













Edward Ngoyai Lowassa alizaliwa Agosti 26, 1953 na katika Kijiji Cha Ngarash huko Monduli, Lowassa ni mtoto mkubwa wa kiume kwa mzee Ngoyai Lowassa.
Kielimu, Lowassa ana Shahada ya Uzamivu (masters degree) katika Maendeleo kutoka Chuo Kikuu Cha Bath nchini Uingereza aliyohitimu mwaka 1984, na kabla ya hapo alihitimu shahada ya kwanza katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1977.

Kikazi, Lowassa amekulia na kufanya kazi zaidi ndani ya CCM na serikali yake. Lowassa amejiunga na CCM akiwa chuo kikuu cha Dar es Salaam. Huko alikuwa mwanachama hai na baadae kiongozi wa Tanganyika African National Union (TANU) Youth League (baadae CCM Youth League). Mara baada ya kuhitimu masomo, aliajiriwa na CCM kama katibu msaidizi na baadaye katibu wa wilaya. Akiwa kijana ndani ya CCM alipata kuwa msaidizi wa Mzee Rashid Mfaume Kawawa, Daudi Mwakawago na Horace Kolimba.

Mzee Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika na Tanzania, mmoja wa waasisi wa chama na taifa letu. Bila shaka Lowassa alijifunza mengi kutoka kwake, na kama sio utiifu wa hali ya juu na uzalendo wake kwa taifa, asingekweza kufanya kazi na mzee Kawawa,anayesifika kuwa na misimamo ya hali ya juu.

Pia Lowassa ni Luteni wa jeshi, licha ya kupigana vita dhidi ya Idd Amin nchini Uganda mwaka 1978/1979, pia akiwa jeshini alifanya kazi kwa ukaribu na Rais Jakaya Kikwete pamoja na katibu mkuu wa CCM wa sasa Mh Abdulrahman Kinana. Wote tunajua kuwa jeshini ndiko kulikobobea kwa kufunzwa uzalendo na utiifu wa hali ya juu.

Mwaka 1985,Lowassa aliteuliwa kuwa Mbunge kupitia Umoja Wa vijana CCM (UVCCM), sambamba na Mama Anne Makinda (Spika wa Bunge la sasa) na Jenerali Ulimwengu. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Monduli akipeperusha bendera ya CCM ambako amekuwa mwakilishi hadi leo.

Toka mwaka 1977 Lowassa amekuwa akiaminiwa na CCM na hakuwahi kukiangusha, amekwisha kabidhiwa dhamana nyingi za uongozi zenye kumpa dhamana ya kusimamia na kutekeleza ilani za chama, nyadhifa ambazo kila wakati alizitekeleza kwa ufanisi wa hali ya juu. Lowassa amekwisha kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania (2005-2008), Waziri wa Maji na Mifugo (2000-2005), Ardhi na Makazi (1993-1995),  Haki na Mambo ya Bunge (1990-1993), na Mazingira na Mapambano dhidi ya umasikini katika ofisi ya Makamu wa Rais.

mwaka 2008 alikubali kwa ridhaa yake kuachia nafasi yake ya Uwaziri Mkuu ili kulinda heshima ya serikali nzima, Chama tawala CCM na pia ili kuepuka mgawanyiko miongoni mwa wanachama, wananchi na viongozi. Huu ni uungwana na uzalendo wa hali ya juu, wenye moja ya vielelezo vya utawala bora.


Mwaka 2014 tumeshuhudia sakata la Escrow ambapo pamoja na kuwa na ushahidi wa wazi wa pesa kwenye akaunti zao, baadhi ya Mawaziri waligoma kuwajibika kwa hiari yao na wengine kusimamishwa kazi na Rais. Lowassa alijiuzuru kwa tuhuma tu, ambazo hazikuwa na mashiko wala ushahidi yakinifu, wala walau kupewa nafasi kuhojiwa na kamati teule ya bunge.hivyo nydhifa ya juu aliyowahi kushika ndani ya serikali ni waziri mkuu wa jamhuri

wa muungano wa Tanzania ambapo Alichaguliwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa

kumi wa Tanzania tarehe 30 Desemba 2005 akajiuzulu tarehe 7 Februari

2008 kwa kashifa ya Richmond. Sasa ni mgombea urais kupitia Chama cha

Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) chini y amwamvuli wa umoja wa 

katiba ya wananchi (UKAWA)

Post a Comment: