Polisi katika eneo la ajali ya chopa ya Filikunjombe
Kamishna
wa operesheni na mafunzo wa Jeshi la polisi, nchini Tanzania Paul Chagonja
amethibitisha kutokea kwa ajali ya helikopta
Nnamba 5YDKK katika eneo la pori la selous kwenye kijiji cha Mtende
mkoani Morogoro iliyosabaaisha vifo vya watu wanne akiwemo mgombea wa ubunge
jimbo la Njombe Deo Filikunjombe.
Wakati Akizungumza na Sauti ya Amerika kwa njia
ya simu jana tokea eneo la tukio kamishna Chagonja amesema maiti nyingine
iliyotambulika ni ya rubani wa helikopta hiyo William Slaa huku abiria wengine wawili ambao ni wanaume
wakiwa bado hawajatambulika.
Filikunjombe ambaye alihitimu shahada ya
uandishi katika chuo kikuu cha Makerere Uganda amewahi kufanya kazi katika
vyombo vya habari nchini Tanzania kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Njombe
katika uchaguzi wa mwaka 2010.
Taarifa za kuanguka kwa helikopta
iliyopoteza uhai wa Filikunjombe aliyekuwa mbunge machachari na makamu
mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali katika bunge lililopita
zilianza kusambaa Alhamisi jioni katika mitandao mbalimbali ya kijamii na
hatimaye majira ya mchana Ijumaa ndio ikathibitika kwamba watu wote waliokuwemo
kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia
Kamishna Chagonja amesema polisi na
taasisi nyingine ikiwemo mamlaka ya usalama wa anga imeanza uchunguzi wa chanzo
cha ajali hiyo ya helikopta ambayo inadaiwa ilikuwa imekodiwa na marehemu Deo
Filikunjombe
naye mwenyekiti wa kamati ya mazishi ambaye alikua ni mwenyekiti wa kamati za hesabu za serikali na rafiki wa marehemu Mh Zitto Zuberi Kabwe amesema tayari miili ya marehemu imeshafikishwa jijini Dar es salaam na kuhifadhiwa katika hospital ya rufaa ya jeshi lugalo na kwakuwa imeharibika sana mazishi yanatarajiwa kufanyika ndani siku mbili zijazo
Deo Filikunjombe anakuwa mbunge wa sita
kupoteza maisha katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu
na hivyo utalazimu pia uchaguzi wa
ubunge kuahiriswa kwenye jimbo hilo.
na ufuatao ndio wasifu wa marehemu kwa mujibu wa ofisi za bunge
|
Salutation | Hon. | Member picture
 |
First Name: | Deo |
Middle Name: | Haule |
Last Name: | Filikunjombe |
Member Type: | Elected Member |
Constituent: | Ludewa |
Political Party: | Chama Cha Mapinduzi |
Office Location: | Box 12707, Dar Es Salaam |
Office Phone: | +255 752 087766/+255 774 776688 | Office Fax: | |
Office E-mail: | dfilikunjombe@parliament.go.tz |
Member Status: | Active |
Date of Birth | 4 March 1972 |
|
| | | | |
Ludewa Primary School | CPEE | 1986 | To Date | Primary School |
Kasita Seminary Mahenge Diocese | CSEE | 1989 | 1992 | Secondary School |
Forest Hill Secondary School, Morogoro | ACSEE | 1994 | 1996 | Secondary School |
Matola Pre-Form One Seminary, Njombe | CSEE | 1988 | 1989 | Secondary School |
CCP Moshi Police Training School, Kilimanjaro | Certificate (Basic Field Craft) | 2000 | 2001 | Certificate |
Center For Foreign Relations College, Dar Es Salaam, Tanzania | Language Course | 2001 | 2002 | Certificate |
Makerere University (MUK), Kampala - Uganda | BA (Mass Communication) | 1996 | 1999 | Masters Degree |
|
| | | |
The Parliament of Tanzania | Member - Ludewa Constituency | 2010 | 2015 |
World Vision International, Tanzania | Communications Manager | 2005 | To Date |
World Vision International, Tanzania | Public Relations Communications Coordinator | 2002 | 2005 |
Public Exhibition, Benchmark Production | Research Assistant | 2002 | 2002 |
Tanzania General Elections | Media Monitor | 2000 | 2000 |
The New Vision Newspaper | Freelance Photographer | 1998 | 1999 |
TAZAMA, Makerere University, Uganda | Communications Manager | 1998 | 1999 |
The Guardian Newspapers, Dar Es Salaam, Tanzania | Columnist | 1997 | 2002 |
Radio One Stereo, Kampala - Uganda | Correspondent | 1997 | 2001 |
National Television, ITV | Stringer | 1996 | 2001 |
|
Chama Cha Mapinduzi, CCM | District Youth Commander | 2009 | To Date |
Chama Cha Mapinduzi, CCM | Secretary (Ludewa District - Economics & Finance) | 2006 | To Date |
Chama Cha Mapinduzi, CCM | Member - Iringa Region Political Committee | 2006 | To Date |
|
D. Filikunjombe: The Role of the Electronic Media in the Campaign against HIV/AIDS in Tanzania | 2010 |
Post a Comment: