Sunday, 25 October 2015



PROF BAREGU MWESIGA

PROF BAREGU : tumezoea swala kubwa katika uchaguzi ni la amani na jambo libnalochangia ni wapiga kura kuoa wametendewa haki.hivyo natoa tahadhari kwamba kama Watanzania watasoma matokeo hayajafanana na watu walivyopiga kura zao HAWATAKUBALI. kisha kukawa  na uwezekano mkubwa na watanzania kukataa matokeo na kusema liwalo liwe.ni wazi tangu jana tumeanza kuona dalili la uchaguzi huu kuharibiwa (rigging) kwa kukamta karatasi ambazo zimeshapigiwa kura.Kama njombe walikamata gari limetiwa moto tume imesema ndio vilikua vifaa hivyo ila vinakupa picha jinsi gani watanzania wanataka haki.Mvomero pia,hapa Dar es Salaam yamekamatwa hii ni mwanzo tu.Na tunaendelea na kusikiliza,ila nataka kuwaonyesha HATARI iliyoko mbele yetu.
PROF BAREGU  : Kuna simu za viongozi wetu zimekua jammed,mimi kwahivyo inita tu kila dakika mbili,hivyo hivyo mwenyekiti freeman mbowe,mrema nakadhalika.Simu zinaita ukipokea inazima .Unaona sasa tumetoka katika uchaguzi tumeingia katika psychology war fare.wakati rais alivyofungua kampeni alisema maadui zetu ni kuwapiga tu,sasa uadui umetoka wapi? Uchaguzi ni ushindani.na kama mchezo unabadilika na kama taratibu zinabadilika wanavyoweza kubadilisha ndivyo na sisi tunaweza kubadilisha.

Akiongea kwenye mkutano huo pia Prof Safari amesema
PROF SAFARI: Tangu Vituo vya Uchaguzi vilivyofunguliwa asubuhi kumetokea matatizo kadha wa kadha.Matatizo haya tunmepigiwa simu na mengine  kuona katika TV Kama tukio la buguruni ilikua direct sio heresay na tumeona waliohusikaKama tunaamini karatasi za kupigia kura zimekutwa mahali mbalimbali na kama inaaminika anaekana na hizi karatasi ni tume ya uchaguzi.
Hii inamaanisha kwanza karatasi zimeibwa au tume imeungana na ccm kuharibu uchaguzi.na matukio yaliyotokea ni ushahidi tosha tume ya uchaguzi  sio HURU na HAKI,ushindi wetu ni tsunami na kuna maeneo ambayo ngome zetu bado matokeo hayajafika.
PROF SAFARI    :  Nimepata taarifa kutoka katesh manyara kwamba kuna vijana kutoka shule ya sekondari NANGWA ambako wamekataliwa na mwl.wao mkuu amewakatalia kwenda kupiga kura.Amewaruhusu wanafunzi 20 pekee.sababu Tume haikuwaandalia wanafunzi wa vyuo mfumo wa kupiga kura ambao walijiandikisha vyuoni na kwa sasa wako majumbani.
PROF SAFARI    : Serikali imetenda hili makusudi na hili la sekondari ni mwendelezo na linahusiana .ila Safari hii kumekua na tatizo nchi nzima la vifaa mfano Kimara stop over na saranga hadi jioni vifaa havikua vimefika.
PROF SAFARI    :Tume ya uchaguzi ilikua imetoa maelezo kuwa vifaa hivyo vilipelekwa jana saa tisa usiku vikaharibiwa na hadi muda huu hawajarekebisha. Bali Polisi wamepelekwa kule kudhibiti watu,wapiga kura wanasubiri vifaa ila wameletewa mapolisi ili kuwaogopesha na sio vifaa.
PROF SAFARI    : Na hata pemba hili limetokea hakukua na karatasi za rais na hata karatasi za kujumlisha matokeo yake.na Voter Register kuna watu wengi wameenda hawakukuta majina yao kama Tanga,Singida,Pemba na Dar.
Naye  meneja wa kampeni wa chama cha demokrasia na maendeleo ndg John mrema akiongea na waandishi mahali hapo amesema
JOHN MREMA   : Mkoa morogoro wametumia mihuri ya mwaka 2010 na Tumesikia maeneo baadhi watu hawajapiga kura na tume imeahidi kuongeza muda nakuna maeneo bado hakuna karatasi za kujumlisha matokeo ya urais pia. Kuhusu suala la kuhesabu  kura haswa mkoani Tanga RC ametangaza kuwa kura zitahesabiwa halmashauri tumesisitiza kuwa ni kinyume cha kampeni.
 kwa maeneo ambayo tayari tumeshapata matokeo yetu yanaridhisha sana.Tumejiandaa tunaendelea na mawasiliano na mawakala wetu mpaka saa sita usiku tutakua tumekusanya kura 70%.Tutakwenda tume na matokeo yetu yaliyokusanywa .
JOHN MREMA   :Tunawatahadharisha kuhusu vituo vyao vya Chang’ombe,oysterbay na kurasini tunapata taarifa ya michezo wanayofanya na bahati nzuri wako wanaopenda mabadiliko katika vituo hivyo.maana waliopiga kura sio polisi na jeshi ni wananchi na wameamua

Post a Comment: