MWANAHARAKATI WA SIASA MKONGWE TANZANIA AUNGA MKONO MABADILIKO 2015
Mwanachama wa siku nyingi na nwanaharakati wa chama kikongwe Tanzania MH KINGUNGE NGOMBARE MWIRU leo mchana akiongea na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari.ametamka wazi kuunga mkono harakati za wananchi wa TANZANIA kutaka MABADILIKO kwa mwaka huu wa 2015.
Akitoa ufafanuzi mzee amesema mabadiliko ndio dhana ambayo wananchi wanahitaji siku zote haswaa,na ndio kitu walichokifanya wao katika harakati zao za maisha tangu ujana wao.akitoa mifano ya yeye,mwalimu nyerere na wengine wengi ambao waliacha kazi ndani ya serikali ya wakoloni ili kuleta mabadiliko Tanganyika na uhuru kupitia Tanu,lakini pia akiongezea hilo mzee Kingunge amesema mabadiliko yaliendelea hata ya uhuru kwa kujenga muungano ndani nchi za tanganyika na zanzibar april 26.na baada ya kuyumba sana kwa muundo wa vyama viwili vilivyokua vikishika nchi vya ASP NA TANU waliamua kufanya mapinduzi ya kimuundo na utendaji ndipo walipoanzisha chama cha mapinduzi.
na ndani ya chama hicho pia walishafanya mabdiliko kadhaa kwa ajili ya wananchi mfano mwaka 1990 wakiongozwa na mwalimu Nyerere walikubali kuanzisha mfumo wa vyama vingi.
Watanzania waleo wanahitaji mabadiliko katika elimu,mabadiliko katika kilimo mabadiliko katika utendaji wa kisiasa na mfumo ambapo chama cha mapinduzi wameshindwa kuliona hilo.matokeo yanayoonekana ni viongozi wa juu wa chama hicho kuanza kubadili kauli mbiu za chama na kujiita chama tawala nasi kubadala ya kudumisha mapinduzi.
Mzee Kingunge anasema kipindi hiki ambacho ana uhakika vijana wasomi wengi wao wanahitaji mabadiliko yeye anashangaa kuona
viongozi wa juu wakilichokua chama chake wanapita majukwaani na kusema hawako tayari kuwakabidhi upinzani madaraka.je hii demokrasia na mfumo wa vyama vingi waliuanzisha wa nini !!??
viongozi wa juu wakilichokua chama chake wanapita majukwaani na kusema hawako tayari kuwakabidhi upinzani madaraka.je hii demokrasia na mfumo wa vyama vingi waliuanzisha wa nini !!??
mwisho kabisa anasisitiza kua yeye anasapoti mabadiliko kwa kua anahitaji mtu ama chama kingine cha kupeeleka tanzania mbele maana miaka 50 ambayo CCM imekaa madarakani ni kama imelevya na madaraka ,na chama kikilevya na madaraka hakuna jipya itakaloweza leta.
Post a Comment: