MKAKATI WA KUIBA KURA WANASWA
* NEC YAHUSIHSHWA. MSIMAMIZI MKUU NI DR. MODESTUS KIPILIMBA
* ALIKUWA MTUMISHI WA BOT, AKADAGANYA KACHUKUA LIKIZO KUMBE KAENDA NEC KWA KAZI MAALUM.
Niliposikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wamekubali matokeo kubandikwa ukutani kwenye vituo husika, niliwaza sana ni jinsi gani CCM inanusurika. Kwa bahati nzuri imegundulikwa kwamba mchezo wote utafanyika kwenye mfumo wa ujumlishaji wa matokeo "Tallying System".
Msimamizi mkuu wa hili zoezi ni Dr. Modestus Kipilimba ambaye katoka BOT (Bank of Tanzania) na kupelekwa ofisi za NEC kwa kile kinachoitwa kazi maalum....
* Dr. Modestus Kipilimba ni nani?..... (Tuanzie hapo)...
Dr. Kipilimba alikuwa mtumishi wa BOT Miaka kadhaa iliyopita. Baada ya kuhusishwa na wizi wa mabilioni ya fedha katika taasisi hiyo alifukuzwa kazi kwa barua namba MFP/BOT/PF/24/03. Baada ya kufukuzwa kazi alikimbilia nje ya nchi (Uingereza) ambapo alienda kusoma zaidi.
Baada ya Prof. Ndulu kuwa gavana wa Bank, Ndugu Kapalimba haijulikani jinsi alivyorudi kazini. Ila ni wazi alipitia mlango wa nyuma, baada ya uongozi wa juu wa banki hiyo kupewa agizo la Dr. Kapalimba kurudishwa kazini. Dr. Kapalimba akaajiriwa tena kwa mara ya pili na kupewa cheo cha "Bank Advisor". Kwa muda mfupi akapandishwa cheo na kuwa mkurugenzi wa idara ya Risk Mgt.
Mwezi uliopita Dr. Kapalimba kwa taarifa zilizopo BOT zinaonyesha Kapalimba kachukua likizo. Ila cha kushangaza huyo bwana yupo anafanya kazi NEC na kapewa idara nyeti ndani ya kurugenzi ya IT. Na pia ni yeye aliyepewa jukumu la kupokea na kusambaza makaratasi ya kupigia kura.
Dr. Kapalimba ni mtaalamu wa IT, aliyepeta elimu hiyo nje ya nchi na ni moja wa watu wanaosifika kwa utaalam huo. Idara nyingi za serikali imekuwa ikimtumia kwa operation mbalimbali...
NB:.. Baada la hili kujulikana sasa tunaomba tume ya uchaguzi ikubali ombi la kaimu katibu mkuu wa CHADEMA, John Mnyika. La kutaka mfumo wa kujumuisha idadi za kura ukaguliwe mara moja na vyama vyoto wakiwemo CCM...
Kukagua mfumo husika ndio suluhu kwa sasa. Ila bila NEC kuruhusu hilo, bao la mkono litakuwa hapo....
C&P
Post a Comment: