Tuesday, 6 October 2015

Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini Tanzania bwana EDWARD LOWASSA jana aliwaaga rasmi wapiga kura wake wa  jimbo lake la nyumbani Monduli.akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika jimboni hapo mh lowassa ambaye alikua mbunge wa jimbo hilo kwa takribani miaka 20 amesisitiza kwa wana monduli kuendelea kuishi kwa upendo,amani na kusaidiana kama ilivyo ada yao.maana kuna maisha yanaendelea baada ya uychaguzi hivyo wale waliokuwa basi moja wakashuka basi wasigongane wala kuzomeana maana wananchi wa monduli wote siku zote ni ndugu na wamoja.

akimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chadema.Mh Lowasa alimaliza zile fununu zote zilizokua zikiendelea chini chini za nani ni chaguo lake katika kurithi kiti chake hicho baada ya kumnadi mgombea huyo wa Chadema.


Mh Edward Lowassa akiingia uwanjani hapo sambamba na waziri mkuu mstaafu Mh Fedrick Sumaye huku wakiwapungia mkono maelfu ya watu waliojitokeza
      Mh Edward lowassa akipokea baraka za wazee wa kimasai

Mh Fedrick Sumaye akisistiza jambo kwa ishara kuashiria mwaka wa mabadiliko.Katika mkutano huu aliweza pokea kadi zaidi ya elfu kumi ambazo wanachama wa vyama mbalimbali ikemo CCM walirudisha kodi zao wabunge nakumuunga mkono
Mama Regina Lowassa naye akionyesha uhodari na ushupavu wake kwa wananchi wake wakati akimuombea kura za urais mumewe
Baadhi ya wasanii maarufu Nchini waliombatana na Mh Lowassa katika kampeni zake wakifuatilia kinachoendelea kwa umakini
 vijana walijitokeza kwa wingi kumshudia mheshimiwa huyo
                          Mama Regina Lowassa
     wakinamama wa kimasai pia nao waliweza kuhudhuria mkutano huo


 Mh Edward Lowassa akihutubia akiwa pamoja na fimbo ya kimila alikabidhiwa rasmi na wazee wakimasai ambao wakuu wa boma mbalimbali
 

Post a Comment: