LOWASSA :NIMEJIAANDAA KUIONGOZA TANZANIA
Mbeya/Mbarali.
Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa amesema amejiandaa na yupo tayari
kuwaongoza Watanzania akiwa rais wa awamu ya tano.

Akizungumza
kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe- Mbeya Mjini, Lowassa alisema: “Ninatosha,
nitumeni kwa kura zenu… nipeni kura za kutosha niwatumikie.”
Lowassa
ambaye alisema anasikia deko kutokana na wingi wa watu, alisema misamaha ya
kodi kwa sasa ni Sh1.6 trilioni na kwamba atahitaji Sh1.3 trilioni kati ya hizo
kwa ajili ya elimu itakayolipiwa na serikali kuanzia chekechea hadi chuo kikuu.
Alirejea
kusema kuwa katika serikali yake hakutakuwa na michango ya elimu, maabara wala
madawati.
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha Lowassa, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema
viongozi waliokuwa CCM akiwamo Lowassa, wamejiunga na chama chao kwa kuwa kina
misingi imara.
Akizungumzia
suala la upigaji kura, alisema siku sita zilizobaki ni muhimu kwa Watanzania
kufanya uamuzi na kusisitiza kuwa kuna kila sababu ya kubakia kwenye vituo vya
kura baada ya kupiga kura huku akidai kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),
haiko huru.
Sumaye:Akihutubia
mkutano huo, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye alimtaka Waziri wa Uchukuzi,
Harrison Mwakyembe kuwasomea wananchi wa Mbeya, ripoti ya Richmond kuona kama
Lowassa anahusika.
“Lowassa
hahusiki, alijiuzulu kwa ajili ya kuwakoa wao na wao wanaendelea kuilipa
Richmond kwa mgongo wa Dowans wakati Lowassa hayupo,” alisema.
Mbunge
wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi alisema tatizo kubwa kwa wakazi wa jimbo lake
ni maji hasa katika vijiji vya Uyole na Mwakibete na kusema kuna kila sababu ya
kuvuta maji kutoka Ziwa Nyasa hadi Mbeya ili kukabiliana na tatizo hilo.
Alisema matatizo mengine ni hospitali na huduma za afya akitaka wapatiwe
mashine za x-ray, CT Scan na umeme wa uhakika.
Ilivyokuwa
mchakamchaka
Kabla
ya mkutano huo, Jiji la Mbeya lilitawaliwa katika hekaheka za mapokezi ya
Lowassa kuanzia asubuhi huku wakazi wakianza kufurika kwenye uwanja huo tangu
saa mbili asubuhi.
Jiji
lilitawaliwa na pilipika za bodaboda na bajaji zenye bendera za Chadema katika
maeneo mengi hususan Barabara Kuu ya Mbeya- Zambia kuanzia Kabwe, Mwanjelwa,
Mafiati, Soweto na Mama John ulikofanyikia mkutano huo.
Wafuasi
wa mgombea huyo walionekana wakirandaranda maeneo mengi ya jiji hilo wakiwa
wamevalia sare za Chadema huku wakipiga deki Barabara Kuu ya Mbeya - Zambia.
Muda
mfupi kabla ya mkutano kuanza, wafanyabiashara walifunga maduka kwenda
kusikiliza sera.
Wachuuzi
wa vyakula na vinywaji walihamishia biashara zao kwenye mkutano huo tangu usiku
wa kuamkia jana na wengi walionekana kufurahia uamuzi wao kutokana na biashara
waliyofanya.
Mmoja
wa wauza chipsi, John Antony alisema: “Aisee si unajua tena kufaa kufaana, leo
kuna neema kubwa kwetu ndiyo maana leo tumehamishia biashara yetu uwanjani.”
Mbarali:Katika
mkutano wa Mbarali, wafuasi wa CUF na Chadema walizua tafrani wakati
wakimsubiri Lowassa katika Uwanja wa Mpira, Rujewa.
Tafrani
hiyo ilizuka baada ya mgombea wa CUF, Gamdust Haji kufika na gari lake kisha
kushuka na wafuasi wanaomuunga mkono kwa kumbeba juujuu na kumpeleka jukwaa
kuu, jambo ambalo liliwakera wafuasi wanaomuunga mkono mgombea wa Chadema,
Liberatus Mwang’ombe na kutaka kumuondoa kwa nguvu.
Polisi wazima rabsha
Baadhi
ya mashuhuda walisema kulikuwa na kundi la wafuasi wanaomuunga mkono mgombea wa
CUF na kundi la mgombea wa Chadema ambao walikuwa wakilumbana huku kila upande
ukitaka mgombea wao ndiye anadiwe na Lowassa kwa wananchi.
“Unajua
hawa watu walishindwa kuafikiana nani agombee ubunge kupitia yale makubaliano
yao Ukawa, kitu ambacho kila chama kilisimamisha mgombea wake,” alisema mmoja
wa wakazi wa Rujewa mjini, Athumani Mwakitalima.
Akizungumzia
suala hilo, Haji alisema: “Ni kweli nimefanyiwa vurugu, wamevunja vioo vya gari
langu, wakitaka niondoke kwenye mkutano huo eti sina haki ya kushiriki na
kumsikiliza mgombea wangu wa urais. Nimetoa taarifa polisi na kuna watu
wamekamatwa.”
Aliwalaumu
viongozi wa kitaifa walioambatana na Lowassa kwamba hawakutaka kuuliza sababu
za yeye kutowapo mkutanoni hapo na badala yake kumnadi Mwang’ombe akisema
hawakutenda haki.

Post a Comment: