Sunday, 25 October 2015



Asalam alyekum

Kama utapata bahati au wasaa kupitia mitandao ya kijamii na kujua kinachoendelea nchi nzima kuamkia siku ya uchaguzi wa madiwani,wabunge na rais . basi hakika utakutana na hii habari iliozagaa sana na kutawala mitandao ya kijamii kwa siku mbili hizi.ni habari inayohusu kukamatwa kwa magari mawili ya serikali moja huko mkoani Njombe,gari mali ya Tanroads na jingine katika jji la Mwanza.lakini pia kule Hanang   kakamatwa mtumishi wa serikali na kada wa chama cha mapinduzi Mh Marry Nagu.
Hakika mwanzoni akili yangu haikutaka kukubaliana na mawazo ya Mh Mbowe na wenzie ya kuhamasisha  vijana wa kitanzania kukaa mita mia mbili (200) walinde haki yao ya msingi isipotee lakini dalili hizi zilizoanz akujionyesha hadharani hakika sasa natambua nini walimaanisha hawa waheshimiwa na kuunga mkono hoja hiyo.
CCM kama chama tawala na kongwe hapa nchini na Africa walipaswa wao ndio wawe kielelezo  tosha cha demokrasia ya kweli lakini pia wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuzuia viashiria vyote vya uvunjifu wa amani hii tuliochiwa na wazee wetu.ila leo hii imekua vinginevyo,chama hicho kikongwe ndio kimeanza kuonyesha rafu mbaya za uchaguzi hata kabla kura zenyewe hazijapigwa.


Nilisikia wakijitetea hawahusiki na mpango wa Mh MARRY Nagu wa kujiandalia kura za wizi ili aweze kushinda.,lakini vip hili la mkoani Njombe amabapo wananchi wamekamata gari mali ya Tanroads ( taasisi ya ujenzi wa barabara iliochini ya wizara ya ujenzi )  ambayo ni wizara inayoongozwa na Mh John P Magufuli (mgombea urais kwa tiketi ya CCM) .
GARI AINA YA LANDCRUISER STK 4599 MALI YA TANROADS LILIOKAMATWA NJOMBE LIKIWA NA KURA ZA MAGUFULI,MKOANI NJOMBE.

kilichokibaya zaidi ni wahusika waliokutwa kwenye gari hilo walipohojiwa nawakadai kuwa wanasafirisha t-shirt zenye ya mgombea huyo  lakini gari lilipokaguriwa ndipo zikakutwa na hizo kura za wizi.  Kwa mazingira haya sijui mtasema nini ambacho watanzania watawaelewa na kuwaamini kua huu ni uchaguzi huru,wahaki na amani

kuonesha dhahiri huu ni mpango wa CCM ambao pia haungwi mkono na watanzania wengi wanaopenda mabadiliko.jioni ya leo tarehe 24/10/2015 masaa machache kabla ya uchaguzi mkuu.mzigo mwingine wa kura feki umekamatwa mjini Tanga ukiwa unasafirishwa kutoka jijini D ar es salaam kwa njia ya basi
PICHA IKIONYESHA MABOKSI YA KUPIGIA KURA YENYE KURA AMBAZO ZIMEKWISHAPIGWA YALIOKAMATWA KWENYE BASI LA TAHMEED MJINI TANGA 



Gari likiteketea kwa moto baada ya wananchi wenye hasira kali  wakazi wa jiji la Mwanza kuliwasha mara punde walipojiridhisha kuwa nalo  liliku limebeba kura za wizi                                                                                                                                                                             

Post a Comment: