KUTOKA MAGAZETINI LEO TAREHE 7/10/2015
Hoja nzito za Lowassa kuelekea Ikulu 2015
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Lowassa, amesema: “Watanzania tuna fursa ya pekee kuuondoa utawala wa CCM madarakani na kuleta mabadiliko ya kweli nchini.” Lowassa amesema hayo, katika salamu zake kwa Watanzania katika kitabu cha ilani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yenye mtazamo wa pamoja wa vyama shirika vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Mbali ya Chadema, vyama vingine vinavyounda umoja huo ni National League for Democracy (NLD), Chama cha Wananchi (CUF) na The National Convention for Construction and Reform – Mageuzi maarufu...JAMHURI MEDIA
Lowassa: Wanajisumbua
Mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, amesema hana muda wa kuwajibu wale wote wanaomsakama, lakini amejipambanua kuwa anataka kuwatumikia Watanzania kuanzia mwezi huu. Lowassa amesema kwa malengo hayo ya kutaka kuwatumikia Watanzania ambao kwa zaidi ya miaka 50 ya Uhuru na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wameshuhudia nchi inakabiliwa na matatizo ya kimsingi ikiwamo rushwa na ufisadi. Miongoni mwa watu wanaomsakama Lowassa ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, anayeelezwa kushika wadhifa huo kwa kazi maalum ya ‘kumtukana’ mgombea huyo...JAMHURI MEDIA
Lowassa na Magufuli, nabii hakubaliki nyumbani
UKIONA nabii anakubalika nyumbani, anasifiwa na kupongezwa, ujue huyo hafanyi kazi zake za kinabiPrivatus Karugendo...RAIA MWEMA
Amani ya nchi mikononi mwa wahariri na Tume
Wiki iliyopita, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliandaa mikutano mbalimbali na wadau wake wakiwamo wamiliki wa vyombo vya habari na wahariri. Katika mikutano hiyo, mengi yamezungumzwa lakini kubwa ni kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini kuagizwa kufuata maadili ya taaluma sambamba na sheria za uchaguzi, ili kuepuka kupitisha habari kutoka vyanzo visivyo rasmi. Mwenyekiti wa Tume, Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu, Damian Lubuva, amewaambia wahariri kwamba wana dhamana kubwa ya amani ya Tanzania sasa, wakati wa Uchaguzi Mkuu na baada ya mchakato huo. Katika wito wake, Jaji... Published By: Jamhuri Media
Post a Comment: