Kuna Njama Za CCM Kuiba Kura Usiku wa Tarehe 24-MBOWE
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema wamegundua njama za kuiba kura
zitakazofanywa na CCM usiku wa tarehe 24 kwa kupita mitaani na kugawa fedha za
kura feki.
Mbowe
alitoa kauli hiyo
jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Ruanda
Nzovwe vilivyopo jijini Mbeya.
Alisema
ili kudhibiti hali hiyo, siku hiyo Ukawa watafanya doria usiku kucha ili
kuhakikisha hakuna fedha zinazogawiwa wala kura feki zitakazosambazwa.
“Nia
ya Ukawa ya kupigania Katiba ya wananchi iko pale pale kwani Serikali ya awamu
ya tano itaipigania kadri itakavyowezekana ili kiu ya wananchi juu ya Katiba
hiyo ipatikane,” alisema Mbowe.
Alisema
pia kwamba, uchaguzi wa mwaka huu ni wa kihistoria kwa kuwa unahusu maisha ya
watu, watoto na utajibu maombi ya Watanzania.
Pamoja
na hayo, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), siyo huru na kwamba wanachama wa Chadema watahakikisha
wanalinda kura zao.
“Kwa
miaka 25 tumepiga kelele tukidai tume huru ya uchaguzi lakini kilio chetu
hakikusikika kwa sababu CCM inajua tukiwa na tume huru, haiwezi kubaki madarakani.
“Kama
tume yetu siyo huru, tuna wajibu wa ziada wa kulinda kura zetu. sheria inasema
huturuhusiwi kusimama wala kukaa chini ya mita 200 kutoka kituoni. Kwa hiyo,
ukihesabu mita 200 kutoka kituoni, una uhuru wa kuwa eneo hilo,
“Jambo
hili limezua hofu ndani ya tume, ndani
ya Serikali, ndani ya CCM na kwa Rais Jakaya Kikwete kwa sababu anasema
tukishapiga kura, tukalale. Sasa namwambia Rais Kikwete ushauri huo akawape
CCM, sisi hatuutaki,” alisema Mbowe.
Alisema
pia kwamba, wanachama wa Chadema na wapenzi wao, hawatafanya fujo bali watakuwa
na ujasiri wa kupiga na kulinda kura zao kwa sababu hakuna anayeweza kuzuia
mpango wa Mungu kwa kutumia askari au nguvu.
Post a Comment: