HOJA TATU ZA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI DHIDI YA KESI YA MITA 200
Tukiwa
bado tuko kwenye headlines za Uchaguzi 2015 stori inayochukua kasi katika
vyombo vya habari pamoja na mitandao ni kuhusiana na wananchi kusimama mita 200
pale wanapomaliza kupiga kura siku ya
tarehe 25, 2015.
Akizungumza
na waandishi wa habari Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Tulia
Ackson..’Mimi siamini kama uamuzi utakuwa umechelewa kwasababu kesi yenye
imechelewa kuja kwa hiyo mimi ninaamini wananchi wafuata sheria watafuata
taratibu watafuata yale waliyoelekezwa
hata kwenye vituo vya kura au chochote
kile watakachoelekezwa’ – Tulia Ackson
‘Kifungu
cha 104 ibara ya ndogo ya kwanza kinayohistoria inayosema kwamba mtu haruhusiwa
kufanya mkutano siku ya Uchaguzi
kiliongezwa 1996 kwa hiyo kabla
hakikuwepo kwasababu hakukuwa na haja ya hicho kifungu lakini kwa kuona kwamba kuna hilo hitaji
hicho kifungu kikarekebishwa kikaongezewa hilo katazo la mtu kufanya mkutano
kwa hiyo kile kifungu cha 104 ibara ya ndogo ya kwanza hakina utata wowote
lakini wananchi wanataka kujua uhalisi ni upi ndio kilichotuleta mahakamani’ –
Tulia Ackson
‘Mimi
ninaona mjadala unaenda vizuri kwasababu upande wa mleta malalamiko
amesikilizwa kwa kirefu mahakamani itapata fursa ya kupima hizi hoja za pande
mbili itatoa uamuzi ambao unaona uko sawa kwa kile kifungu kinachobishaniwa na
pia kwa mujibu wa katiba, kisheria anayepaswa kulinda kura ni polisi na kifungu
cha 72 kimesema wazi’ – Tulia Ackson
CHANZO :Millardayo blog
Post a Comment: