HIGHNESS KIWIA KUPINGA MATOKEO YA UBUNGE ILEMELA MAHAKAMANI
Aliekuwa
Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba
ya Wananchi Ukawa Highness Kiwia, anatarajia kufungua kesia ya kupinga matokeo
ya uchaguzi jimboni humo kwa madai kwamba haukuwa wa huru na haki kutokana na
kugubikwa na changamoto mbalimbali.
Kiwia
ambae ameshindwa kutetea jimbo hilo baada kuchukuliwa na Angelina Mabula kutoka
Chama cha Mapinduzi CCM, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari
kuhusiana na Uchaguzi huo.
Alieleza
kuwa katika vituo mbalimbali jimboni humo kulikuwa na makosa mengi ambayo ni
pamoja na uwepo wa vituo hewa, idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya
waliojiandikisha katika daftari la kupigia kura pamoja na majina ya wapiga kura
kukutwa katika majimbo tofauti na yale waliyojiandikishia.
Katika
hatua nyingine Kiwia alikanusha taarifa kuwa alimtuma mwakilishi kwa ajili ya
kusaini fomu ya matokeo kwa niaba yake na kwamba siku ya kutangaza matokeo
alishindwa kupokea matokeo hayo na hivyo kuzilai.
Kwa
upande wake Tungaraza Njugu ambae ni Kiongozi wa Kanda ya Ziwa Victoria
Chadema, alisema kuwa zoezi la uchaguzi mwaka huu linapaswa kulaaniwa kwa kuwa
halikuendeshwa kidemokrasia kutokana na kukiuka taratibu mbalimbali za
uchaguzi.
Katika
Matokeo ya Kiti cha Ubunge Jimboni Ilemela, Mgombea wa CCM Angelina Mabula
aliibuka mshindi baada ya kupata kura 85,424 na kufuatiwa na mgombea wa Chadema
Highness Kiwia aliepata kura 61,679 ambapo kwa upande wa Madiwani CCM ilishinda
Kata 16 huku Kata Tatu zikichukuliwa na upinzani.
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema
Post a Comment: