Monday, 5 October 2015


Naam waungwana ,habari za juma ya wiki !? vip huko mtaani kwenu ile habari ya mvua za elnino imeshaanza kujionyesha ama la !? huku kwetu katika mtaa wa siasa kama ni elnino,basi elnino yetu ilikua ni msiba wa wanaharakati wa mtaa.

Msiba wa kwanza ni wa Yule Ndg Kingunge nguli wa harakati za uzalendo kwa miaka zaidi ya 61 alipokikimbia chama alichokijenga na kukilea kwa miaka yote ya maisha yake sababu kimepoteza muelekeo na sifa za kuongoza taifa,na yeye binafsi  kutangaza rasmi kusapoti ule upande wa wananchi wanaohitaji mabadiliko.hivyo basi uamuzi wake umeacha na kupeleka kilio cha msiba kwa wale ndugu wana familia  ya kijani

Huu msiba wa pili hakika umenitia simanzi kubwa sana mwana hekaya sababu ,ndugu yangu huyu alikua jasiri,shujaa na mwanaharakati wa kweli aliyesimama katika kila alichokiamini yeye siku zote na mungu ailaze mahali pepa peponi roho yake mchungaji Christopher Mtikila.AMINA

Pamoja na elnino hiyo kubwa haikuzia kwenye baraza la mtaa kupata mawazo mapya na yakinifu kutoka kwa wana jumuiya.na leo hacha mie niliwakilishe hili lilozua tafrani

Hakika katika jamii yoyote ile duniani jamaa akishaonekana mwizi,mlafi na si muaminifu huwa hatumwi wala kuagizwa jambo lolote kubwa lenye thamani na kuhitaji uaminifu.

Sasa wale ndugu wana jumuiya wa upande wa pili wanapokaa na kusema eti huyu wa upande huu  ni mwizi hafai kuaminika je wamefanya tafiti yakinifu kweli !?

Maana wanapenda sana kumsingizia baba yetu mkuu,ambaye udaktari wake kifalsafa hakumuondoa kwenye hadhi yake ya ualimu lakini wanasahau kuwa ni huyu huyu ndie aliyemtuma kijana huyo akamchukulie tunzo zake za heshima.enzi akiwa katibu mkuu msaidizi wa chama tena hebu tazama yupo waziri wa mambo ya nje ambaye sisemi mengi juu yake lakini mwalimu akamuamini katibu huyo wa chama.
TIZAMA PICHA HII

Halafu ndugu zangu mbona mmesahau kua huyu mwenzetu anaaminika zaidi kuliko huyu mnayemuona mchapakazi na ndio maana mwenyekiti wenu aliamua kumpa utendaji mkuu wa serikali ili aweze hata kumuongoza huyo mnayesema mchapakazi!?

Tulikua na waziri ambaye huhusika ma masuala ya nje na ushirikiano wa kimataifa ambapo kwa miaka 10 wa utawala wa Yule kipara ambaye mnamheshimu sana japo ni bingwa matusi na sasa naye ni mkuu wa kaya .hakuaminika hata chembe mbele ya kipara kwenda kuchukua ama kumuwakilisha kwenye tafrija kubwa zilizohitaji mtu makini zaidi ya kua ni waziri wa kwenda UN  kushangaa wanamuziki lakini akamuamini waziri wake wa maji kwenda kuwakilisha kwenye suala linalohusu ushirikiano wa kimataifa na mikataba ya kitaifa na mwisho akamletea ushindi kwa wananchi wake na leo wanafurahia matunda hayo kwa kunywa maji safi.hakuishia hapo alimpa uenyekiti wa kamati kwenda kufanya tafiti kwa nchi za wenzetu ni jinsi gani twaweza piga hatua.kumbuka yupo waziri wa mambo ya nje na ushirikiano na maagizo yanapita tu mbele yake

Naomba nihitimishe tu kwa kusema kama viongozi watatu wa taifa hili kati ya wanne waliweza muamini na kumtuma kwanini wewe usimuamini akakuongoza!?na unakaa kumuita mwizi pasipo shahidi pia ilhali wajua fika mwizi haaminiki na hatumiki.
ASUBUHI NJEMA









Post a Comment: