HEKAYA ZA MTAA: MAGUFULI USIPIME KWA MACHO
“Asamehewe Yule aliyejua maana ya
msamaha na akamaanisha toka moyoni wakati akiomba msamaha” haya wahenga huita
maneno ya busara lakini yenye haki ndani yake.inatupasa kukumbushana misemo
kama hii hasa kipindi hiki tunachoelekea cha uchaguzi mkuu wan chi yetu ilhali
tukiwa tumebakiza wiki mbili tu.Na wahanga wakubwa ni sisi wakazi wa mtaa huu
wa siasa
Mwisho wa wiki huu na matukio mengi na
yenye kuteka sana hisia hasa wana familia kwakua muda mwingi tunashinda na
familia zetu na kujua matatizo yanayotukabili.nikiwa na vijana wangu tukipata pilau la mchana wa
jumapili ndipo waliponiuliza swali hili “mbona mzee wa push up hajaonekana
mtaani siku ya pili leo ??” kwanza walinishtua maana sikuzani kama vijana wangu
watakua makini namna hiyo lakini pia sikua na jibu kamilifu la swali lao,hivyo
nikawaomba niwasiliane na wajomba zao ambao tumeoleana ndoa ya kudumu katika
familia mabadiliko ila wao ni wazaliwa wa familia ya mkwere.
Nilioyapata kuyajua huko ndio
yamenifanya nione umuhimu wa kuwashilikisha vyema,ndugu zangu ule msemo wa
wahenga usipime kwa macho kumbe una maana nzito hivyo.eti Yule bwana pamoja na
mbwembwe zote zile za push up,kuruka kwenye gari,kukimbia stejini na kucheza
mziki wa yamoto kumbe ni mzee wa mbio fupi marathon haziwezi !? sasa nikawa
najiuliza hawa wenzie ambao kila siku wanashinda majukwaani kumpamba mara oooh
huyu Usain Bolt mara oooh huyu miraba mine hakuna kitakachomshinda kumbe
hawajui mwenzao ni mzee wa mbio fupi ? ona sasa wamemkimbiza tu nusu marathon
anahemea juu juu siku mbili zote hizi haonekani.wakati Yule waliomdharau na
kumdhihaki sasa ndio mwendo mdundo anaongoza marathon kwa mbwembwe zote.
ILA YOTE KHERI KAMA YU MZIMA NA NAMUOMBA KUMPA USHAURI WA BURE HAYA MAMBO SIKU NYINGINE USIPIME KWA MACHO
Post a Comment: