Saturday, 3 October 2015



Asaalamu waungwana, naona kumekucha tena na zimebaki siku 23 kumjua mrithi wa mkwere.

Leo sitokua na nakuu kutoka mtaani maana wamenipa salamu za jaji lubuva nizipeleke magogoni.

Ndugu mkuu wa kaya, vijana wako wameniagiza wanaomba uwakumbuke wao sana sana pale mtakapokaa na jamaa zako wa NEC kumpitisha rais ajaye baada yako maana wanaipenda Tanzania na hawataki kukupeleka ICC
Lakini pia mkuu vijana wanaomba sanasana yale magari yako yenye maji ya washa washa yasizunguke mtaani kutusumbua na kutuonea bali mapema kabisa uwatafute hao mliowapa kadi za NEC zisizo halali.

Mh sana mkuu wa kaya .jamii ya mtaa wa siasa inaomba upokee hizi salamu za jaji lubuva na umwambie sheria ni msumeno hivyo kama lema aliwekwa ndani kwa kuzidisha dk 6 basi angalau hata kwa dakika kadhaa muweke ndani magufuli na wenzie kwa kuwa ni mabingwa wa kuzidisha muda.

Lakini pia aache mara moja kuwa msemaji wa chama cha mapinduzi ilhali veye sio nape bali yeye ni refa wa huu mchezo na atumie sheria zote 17 za mchezo kuchezesha,masuala ya kesi kuletwa kwake (mfano kesi ya bulembo ) na kutoa hoja nyepesi nyepesi katika majibu si sahihi.

Post a Comment: