Thursday, 15 October 2015


 JENERALI DAVIES ADOLPH MWAMUNYANGE


Habari wapendwa

Katika hekaya za leo,mzee wa hekaya amedokezwa kuwa Yule mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini Tanzania,Jenerali Davies Adolph Mwamunyange atawasili leo kutoka ughaibuni.

Taarifa za awali zilionyesha kuwa mkuu huyo ambaye ameleta taharuki kubwa wananchi kwa wiki kadha sasa baada ya kusemekana yu mahatuti baada ya kunywa kitu kinachodhaniwa ni sumu.angewasili nchini leo saa saba mchana,lakini zikaja taarifa zaidi atawasili masaa mawili baadaye.

Na hadi mnyetishaji huyo akimpa habari mkuu wa hekaya za mtaa ni kwamba Jen Mwamunyange alikua hajawasili nchini ila kwa habari za ndani zaidi alikua mahali kusubiri mapokezi ya kuingia nchini kwa utaratibu ambao jeshi letu la ulinzi na usalama  wenyewe wanaona unafaa kuandaliwa



Ikumbuke kuwa taifa kwa ujumla liko katika shauku kubwa ya kumshuhudia kamanda wetu huyo akijitokedha hadharani baada ya kuwepo tetesi za kua ni mgonjwa na wengine kufika mbali na kudai tayari alishaaga dunia.habari ambazo zilichombezwa na kukamatwa kwa mwanafunzi anayesadikiak kua ndio muanzilishi wa habari za kudhuliwa na sumu kwa mkuu wa majeshi huyo.lakini taarifa hizi zimechukua taswira mpya ya kisiasa zilizochagizwa na uchaguzi mkuu wa rais,wabunge na madiwani. kiasi ambacho upo upande unaamini kuwa kamanda huyu mkuu wa majeshi Tanzania ni kweli amenyweshwa sumu katika minijali ya kumdhuru baada ya kuonesha msimamo wake nje ya ule wa serikali na ndio sababu iliompelekea kwenda nje ya nchi kwa matibabu zaidi,lakini pia serikali na familia vikisisitiza kuwa kamanda huyo yuko mzima salama salmin na yuko nje ya nchi kwa kazi maalumu aliogizwa na rais na serikali.

Kwa kipindi chote hicho haya yakiendelea jeshi letu la ulinzi na usalama kupitia msemaji wake mkuu na idara ya habari ya jeshi hilo hawajatoa kauli yoyote ile,hali ambayo imezidisha utata na kuwaweka wananchi njia panda ya nini kile haswa kinachoendelea !?


Mzee wa hekaya za mtaa yeye anaomba arudi tu salama hii leo tumuone na azungumze nasi ili wananchi tuwe na amani moyo na yeye aweze endelea kutulindia mipaka na usalama wan chi yetu mama pendwa TANZANIA ila na kama yupo mtu alijaribu kumtenganisha kamanda wetu na sisi basi ashughulikiwe ipasavyo. 

Post a Comment: