Thursday, 8 October 2015




 
Report za wachumi zinasema tanzania inapoteza bilion 4 kila siku kutokana na foleni (shilingi bilion 4) hebu fikiria hii pesa inayopotea ingesaidia nini kwenye uchumi wetu ingejenga madawati wangapi,zahanati ngapi kila siku.lakini jiji linaloongoza kwa msongamano dar es salaam halmashauri za hili jiji zimepiga kimya kila siku hela ziendelee kupotea

sasa hivi nyumba nyingi za dar za kima cha kati kwenda cha juu kuna magari 4 uani yamepakiwa asubuhi baba,mama watoto wote watatoka na magari kuelekea sehemu hizi kariakoo,posta ndo kwenye maofisi mengi.ina maana kwa siku maeneo haya makubwa ya mjini yanapatwa na magari madogo sio chini ya laki 2 yanaingia mjini hii inaleta msongamano wengi wanatoka na magari binafisi sababu magari ya public hayaaminiki usafiri sio salama.

maono yangu kusaidia kupunguza foleni na kuokoa haya mabilioni kumbuka kwa mwaka ni zaidi ya trilioni 1.4 tsh

1.kuboresha usafiri wa mabus kuwe na mabus ambayo ni ya quality level seat kupeleka watu makazini na kurudisha jioni

2.ikiwa watu wataendelea kutoka na gari ndogo zijengwe sehemu mahalumu tuseme wakazi wa mbezi ya kimara,kibaha wawe na sehemu ya kupaki magari ubungo kama utavuka zaidi ya ubungo utalipia 5000 kwa siku kuingiza gari lako mjini

3.zijenge reli kuanzia maeneo haya kibaha-posta,tegeta(bunju)-posta,mbagala-posta hii itamaliza msongamano watu wengi watapanda treni na kuacha magari madogo nyumbani

4.kuhamisha malori yasipite mjini tena hii itakua na plan kubwa kuiendeleza kisarawe kwa kujengwa bandari ya nchi kavu na kuboresha barabara ambayo itatokea hadi maili moja hapa pia tutatanua mji wa kisarawe kuanzia barabara,ajira za kwenye migahawa ambayo itafungiliwa njiani.hili lilitokea siku moja roli lilipata ajali maeneo ya kibamba tulitumia masaa 6 kwenye foleni ndo unafika nyumbani.zile bandari zote za nchi kavu zitaamia kisarawe mzigo baada ya kupakuliwa bandarini utabebwa moja kwa moja kwenye bandari ya nchi kavu hapo malori yatakuja na kupakia.

Sijaona bado mradi wa mabasi ya mwendo kasi utapunguza vipi foleni sijaona bado.

faida ya kufanya haya.
1.halmashauri za wilaya zote ilala,kinondoni,temeke kuongeza mapato kutokana na makusanyo ya parking za magari tozo la kuingia mjini na gari yako binafsi.
2.kuhifadhi hizo bilioni 4 zinazopotea na kuongeza na bilioni 6 nyingine za kukusanya mapato kama foleni itapungua na kuisha ina maana tunaweza tengeneza bilioni 10 kwa siku kwa mwaka ikapatika zaidi na trilioni 3.6 hebu jiulize pesa kama hiyo ingesambaza maji kwenye jiji la daresalaam,ingejenga barabara ngapi tanzania kwa mwaka,shule zahanati.
3.kupanua wigo wa ajira kwenye treni,kwenye bandari ya nchi kavu kisarawe njia mpya ya malori mashell yatajengwa,mahotel zoe ajira hizo.

mwisho nashangaa baadhi ya watanzania ambao walishangilia mapinduzi ya burundi jana ambayo hajafanikiwa kuchafuka kwa burundi kuatuathiri sisi kiuchumi mpaka sasa tumepokea wakimbizi 17000 kigoma hawa wakimbizi wataharibu mazingira ya kukata miti ili kuweka makizi.

lakini pia inakua ni ngumu kufanya kazi na mtu ambaye anapigana mipaka ilifungwa jana burundi tunajua nchi ambayo haina bandari inategemea vitu vingi kutoka kwetu kutokuwa kwao salama ina maana ni ngumu kufanya biashara kama gari ya mzigo ilikua uiende burundi haitakwenda.

Post a Comment: