Friday, 2 October 2015

  


IKIWA ZIMEBAKI SIKU 24  WATANZANIA WAAMUE  JUU YA NANI WANAMUHITAJI KUWA RAISI WA JAMHURI YA MUONGANO WA TANZANIA.MGOMBEA URAIS KUPITIA TIKETI YA CHADEMA MH EDWARD NGOYAI LOWASSA LEO ALIWAONGOZA WAJUMBE WA CHAMA HICHO NA WANANCHI WA JIJI LA DAR ES SALAAM,KUTOA TAMKO DHIDI YA SERIKALI NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) . TAMKO LILILOPEWA JINA LA KUJULIKANA KAMA TAMKO LA KAWE.
AKIANZISHA TAMKO HILO ,MWANASHERIA MKUU WA CHADEMA MH  TUNDU LISSU (MB) ALISEMA “KWAKUWA KATIBA HII HAIJATOA MUONGOZO WA JINSI  GANI RAISI ANATAKIWA KUKABIDHI SERIKALI. TUNAMUOMBA  RAISI KIKWETE ATOE TAMKO NI LINI NA NI VIPI ATAKABIDHI SERIKALI MAANA TUMESIKIA KINA BULEMBO WAKISEMA, CCM HAWAKO TAYARI KUTUKABIDHI SERIKALI..JE NI KWELI TAMKO LA BULEMBO NI TAMKO LAKO MHESHIMIWA!?”
KATIKA KUSISITIZA HILO MH JOHN MNYIKA ALIOMBA TUME YA JAJI LUBUVA ISEME NI LINI WATAALAMU WA TEHAMA WA TDC NA CHADEMA WATAHAKIKI DAFTARI LA WAPIGA KURA
NA KATIKA KUPIGILIA MSUMARI WA TAMKO LA KAWE MH HALIMA MDEE SAUTI YA ZEGE  ALISEMA NEC WANAJUA WANACHOFANYA NA WANAJARIBU KAMA KUONA  JAMII ITASEMAJE , LAKINI PIA KAMWE CHADEMA ISIKUBALI UHUNI WA NEC WA KUDAI KWAMBA KILA MWENYE KADI YA KUPIGA KURA ATAPIGA KURA KWASABABU CCM NA NEC WAMETENGENEZA KADI NYINGI FEKI.
KATIKA KUHITIMISHA HILO MH EDWARD LOWASSA AMESEMA TAMKO LA KAWE NI ZITO NA MUHIMU SANA WAKE NA YEYE AMELICHUKULIA KATIKA UMUHIMU HUO HUO HIVYO WAMUACHIE YEYE ATALIFANYIA KAZI IPASAVYO.

Post a Comment: