CCM DODOMA Kuzuia Wanafunzi Wa Vyuo Wanaosafirishwa Kupiga Kura
Chama
cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma kimesema kuwa kimejipanga kuhakikisha
wananchi ambao sio wakazi wa maeneo husika mkoani humo hawashiriki kuwachagua
viongozi wasiowahusu.
Katibu
Msaidizi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Othman Dunga aliyasema hayo hivi karibuni
alipoongea na waandishi wa habari mkoani humo, ambapo alieleza kuwa wanafunzi
wa vyuo vikuu mbalimbali waliojiandikisha katika mkoa huo lakini hawaishi
maeneo hayo hawataruhusiwa kupiga kura kuwachagua wabunge na madiwani.
“Zipo
taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Ukawa wameanzisha utaratibu wa kukodi
magari kwa ajili ya kuwaleta wanafunzi ambao wamejiandisha hapa kwa ajili ya
kupiga kura. Huu ni ushahidi tosha kwamba sio wakazi wa Dodoma,” alisema Dunga.
“CCM
tumejipanga kuhakikisha hawapigi kura za kiongozi asiyewahusu, mawakala wetu
watakabidhiwa orodha ya wakazi na wataisimamia hiyo,” Dunga ananukuliwa.
Kulikuwepo
na taarifa zisizo rasmi kuwa kuna ‘wasamalia wema’ ambao wamejitolea
kuhakikisha wanafunzi wa vyuo vikuu waliojiandikisha katika daftari la wapiga
kura wakati wakiwa vyuoni na sasa wako majumbani, wanarudi katika maeneo
waliyoandikishwa ili wapige kura.
Kwa
mujibu wa Dunga, huenda wanafunzi hao wakaambulia kupiga kura kumchagua rais
pekee katika eneo walilojiandikishia walipokuwa wanasoma vyuoni hapo.
Post a Comment: