CCM NA MABADILIKO BILA MKAKATI
Wagombea wa vyama vikuu vinavyowania Ikulu ya Taifa vimeibeba juu kwa
juu kauli mbiu ya mabadiliko huku upande mmoja ukishindwa kuainisha mkakati dhahiri wa
kuyafanikisha mabadiliko hayo na pia bila kuyafafanua ni mabadiliko ya
aina gani. Nionavyo kibinafsi kwa upande wa sisiem wanajaribu
kutuaminisha kuwa mkakati wao unaitwa Magufuli. kuwa Mikopo ya wanafunzi, tusubiri Mgufuli aingie; madawa hospitalini, tusubiri Magufuli aingie;
uonevu mama ntilie na machinga, tusubiri Magufuli aingie; uonevu na
kubambikia kesi, tusubiri Magufuli aingie. hivyo wanataka tuaminisha Magufuli amekuwa ilani, sheria
na katiba ya nchi. Mimi naona kama hiki ni kichekesho; sioni ni kwa
vipi mwanadamu anavyoweza kuwa mkakati mahususi wa kumaliza matatizo ya
Taifa zima; ni kwa vipi ataweza kuwepo kila mahali kwa wakati wote; na
pia huyu ni binadamu anaweza kuugua au kupatwa na jambo lolote sijui
hapo tunaenda wapi tena. Mkakati ni mbinu inayokaa kimaandishi na
inayokuwa na nguvu zote za kisheria kuadabisha na kuwajibisha na wala
si kwa kutumia akili ya mtu mmoja na kutegemea leo kaamkaje.
Kwa upande
wa upinzani mkakati wao ni maadili na ulinzi wa rasilimali
za nchi unaoasisiwa na katiba ya wananchi, ingawa nao hawaonekani kuwa
na ujasiri kamili wa kulisimamia hili waziwazi na hivyo kutuacha kidogo naswali hivi mabadiliko tunayoyasikia yanatofautiana au yanafanana.
Labda wao wanamaanisha mabadiliko kwa maana ya kuhama chama cha siasa au
kuiondoa sisiem madarakani na kuleta hali bora zaidi za kimaisha;
lakini yote haya yanawezekana kwao bila hata kuweka hadharani mikakati mahususi ya
kuliwezesha hilo kwasababu dhamira yao inajulikana ni nguvu ya umma.
tofauti na ccm ilioamua kuwachanganya wapiga kura ili wajionea
kwamba wote upinzani na ccm ndio walewale wala hamna tofauti na huenda hamna jipya ni
porojo tu zilizozoeleka ili kupunguza imani ya jamii kwa ukawa.
Post a Comment: