Saturday, 10 October 2015














habari zilizotufikia hivi sasa kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari ni kua jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam wamezuia mkutano wa Mke wa mgombea urais kupitia CHADEMA,Mama Regina Lowassa pamoja na baraza la wanawake chadema (BAWACHA) Ambao ulipaswa kuanza na matembezi ya amani kuliombea taifa amani.

Akiongea na blog ya siasaleotz msemaji huyu anasema mkutano huo ulikua halali na walipewa kibali cha kuufanya siku ya leo lakini ghafla leo asubuhi kamanda mkuu wa kanda ya dar es salaam ,Kamanda Kova alifikia mahali hapo akiwa na vijana wake  na kutoa amri ya kuzuia mkutano huo pasipo kua na maelezo ya kutosha zaidi.hali iliopelekea kutoeleweka hivyo kuleta mabishano na baadhi ya wajumbe wa BAWACHA hivyo kuwakamata akiwemo mwenyekiti wa baraza hilo.hadi habari hizi zinaenda hewani wajumbe hao walikua bado hawajaachiliwa na polisi.

Post a Comment: