BREAKING NEWZ: KINGUNGE aachana na chama cha mapinduzi
Mh Kingunge Ngombare Mwiru
Kada na mwanachama nguri kuliko wote ndani ya CCM Mh Kingunge Ngombare Mwiru ameongea na waandishi wa habari hivi punde.kuelezea msimamo wake na hali ya kisiasa nchini hivi sasa.
akianza kikao hicho Mh Kingunge amesema kwa miaka 61 ya harakati zake za siasa,yeye ni mwanachama pekee aliye hai kwenye harakati ukimuacha Mh ally sykes ambaye ni miongoni mwa wale 17 waanzilishi wa Tanu .lakini pia akiwa muasisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).Anasema ccm ilianzishwa kwa ajili ya mapinduzi ya kimuundo na utendaji wa vyama viwili vya TANU NA ASP.
Akizungumza kuhusu hali ya sasa,amesema kwanza kabisa mchakato wa CCM ulikua ni batili ikiwa na maana kwamba haukufuata utaratibu wa kawaida wa chama.Mzee Kingunge amesema wazi utaratibu wa chama chao ni kwamba wagombea wote ambao hujaza fomu huitwa mbele ya kamati kuu na halmashauri kuu kuhojiwa mmoja baada ya mmoja na sio kama kuteua yenyewe bila kuwaona na kuwasikiliza kama ilivyofanyika hivi sasa.hivyo ukilinganisha mwaka 1995,2005 na mwaka huu 2015 ni hakika ubatili umejitokeza na yeye katika historia yake pale anapoona katiba inachezewa,inavunja ama inaelekea kuvunjwa huwa na tabia ya kusema waziwazi.
akitoa mfano 1972 akiwa mkuu wa mkoa wa singida.katiba ilikua inatakaa mbunge wa kuchaguliwa akiteuliwa kuwa mkuu wa mkoa anatakiwa aachie ngazi mara moja lakini yalipokuaja mabadiliko mapya ilibidi ajiulize kwanini mabadiliko hayo wligundua wapo mawzairi na wabunge ambao raisi aliwahitaji kuwa wakuu wa mikoa na ndio maana wakaaanda rasimu hiyo ambayo walipokaa kwenye kikao cha wabunge wa TANU chini ya mwenyekiti Marehemu Mh Kawawa.wabunge wengi walipinga kwa kuwa walitaka kulinda maslahi yao lakini yeye alipinga kua sio utaratibu na msimamo wake ulipelekea rasimu kurudishwa bungeni ambapo kwa mara ya kwanza serikali tena chini ya chama kimoja ikashindwa kupitisha azimio lake.
kutokana na hali hii aliambiwa na ameiangusha serikali na atafukuzwa kazi na aliongea na mwalimu nyerere akiweka msingi na msimamo huo.na aliachishwa kazi kesho yake.
hivyo yeye binafsi hakubaliani na kilichofanyika julai 11 Dodoma, sababu kilichofanyika ni udhalilishaji na kuwajibisha wagombea wote 38,maana tu ndani ya katiba ya CCM kila mtu anastahili heshma na utu wake.
kibaya zaidi ni kuwa hao wagombea wote wamekaa kimya kasoro Prof Mwandosya,hivyo anawapongeza Mh Nchimbi,Sophia Simba na Kimbisa kwa kufichia maovu yaliotendeka japo sasa wanayumba saana
Akihitimisha anasema kwakuwa uongozi wa chama cha mapinduzi umeamua kukibinafsisha chama cha mapinduzi kwa maslahi yao wenyewe na vijana wanatumika kuwadhalilisha watu.yeye anasema Hakubaliani nao na hicho sio chama walichoshirikiana kukijenga na kuanzia leo Yeye KINGUNGE anaachana na chama cha mapinduzi,kwakuwa si chama tena kinachoheshimu katiba.
Post a Comment: