UHUSIANO WA MASUALA YA UTAMADUNI KATI YA TANZANIA NA CHINA WAENDELEA KUBORESHWA
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga
(katikati) akimsikiliza Afisa Balozi wa China anayehusika na masuala ya
Utamaduni nchini Tanzania Bw. GAO WEI (wapili kushoto) walipofika
katika ofisi za Wizara kutambulisha uongozi mpya na kutoa nafasi kwa
uongozi wa zamani kuaga Wizara yenye dhamana na masuala ya Utamaduni leo
Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga
(kulia) akimkabidhi Afisa Balozi wa China aliyemaliza muda wake katika
masuala ya Utamaduni nchini
Tanzania Bw. LIU DONG zawadi ya picha ya Tingatinga kama ishara ya
kumpongeza kwa kuhamasisha mahusiano mazuri ya kiutamaduni kati ya
Tanzania na China leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga
(kulia) akiangalia vitu mbalimbali vya kiutamaduni alivyokabidhiwa na
Afisa Balozi wa China aliyemaliza muda wake katika masuala ya Utamaduni
nchini Tanzania Bw. LIU DONG (katikati) leo Jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Afisa Balozi wa China anayehusika na masuala ya Utamaduni
nchini Tanzania Bw. GAO WEI
Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo



Post a Comment: