Rais Kikwete kuzindua onesho la Utalii la Swahili International Expo
Kaimu
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Devotha Mdachi (kulia)
akizungumza jana Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya onesho la Swahili
International Expo linalotarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba
Mosi hadi 3, mwaka huu katika ukumbi wa mlimani City Dar es
Salaam.Kushoto ni Meneja wa kampuni ya fastjet Jimmy Kibati kama mmoja
wa wadhamini.
Mratibu
wa onesho la Swahili International Expo Philip Chitaunga (kulia)
akizungumza Dar es Salaam jana kuhusu onesho hilo linalotarajiwa
kufanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba Mosi hadi 3, mwaka huu katika
ukumbi wa mlimani City Dar es Salaam.Wenginekutoka kushoto ni Meneja wa
kampuni ya fastjet kama mmoja wa wadhamini, Kaimu Mkurugenzi TTB Devotha
Mdachi na Milat Mekennon kutoka shirika la ndege la Ethiopia.
ONESHO la Swahili International Expo linatarajiwa
kufanyika wiki hii, kuanzia tarehe 1-3 Oktoba,2015 katika ukumbi wa
Mlimani City ambapo Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Hii ni mara ya pili kwa Onesho hili kufanyika,Mwaka jana ilikuwa mara ya kwanza October 1- -4,2014
Onesho
la mwaka jana liliweza kuwavutia Waoneshaji 40,Mawakala wa Utalii
walioalikwa kutoka nje ya nchi 19 (hosted Buyers),Waaandishi wa Habari
kutoka nje ya nchi 4 (media),Wageni waliotembelea onesho hilo
1,200,Wadhamini 40 na Mdhamini mkuu alikuwa Ethiopian Airlines
Mwaka
huu Waoneshaji ni 100,Mawakala wa utalii na waandishi wa habari
walioalikwa 43, Wageni wanaotegemewa kutembelea onesho 2,000,Wadhamini
41 na Wadhamini wakuu wamegawanyika katika makundi.
Kuna Platinum Category ambao ni Ethiopian Airlines – Mdhamini Mkuu (usafiri kwa ajili ya mawakala wa nje walioalikwa)
Pia kuna Gold Categoryambao ni Fast Jet Airline
Limited, An’gata camps Ltd, FB cars Ltd, Gibbs Farm,Ramada Resort Dar
es ssalaam, SAA North America, Seacliff Hotel, Sopa Lodges and Spicenet
Tanzania .
Kwa upande mwingine kuna Silver
category ambao ni Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,
Antelope Tours and Safaris, Azam Marine, Congema Tours and safaris Ltd,
Fernandes Tours & safaris, Melau Tours & Safaris Ltd, Precision
Air Services, Shirika la ndege la Qatar, Rwandair, Shirika la ndege la
Afrika Kusini , Shidolya Tours & Safaris Ltd, Sun Tours &travel
Lts and Shirika la ndege la Uturuki.
Wengine
ni BougainvillaSafari Lodge, Ledgar Plaza Hotel, Cenizaro Hotels &
Resorts, Emerald Collection Zanzibar, Essque zalu Zanzibar, Holiday Inn
Dar es salaam, Kudu Lodge, Kunduchi bBeach Hotel, Manyara Wildlife
safari Camp, Maru Maru Hotel, Mberesero Lodges & Tented Camps, Melia
Zanzibar, Neptunes Hotels, New Africa Hotel, Ocean Paradise Resort
& Spa, PlanHotel Hospitality Group, Protea Hotel Courtyard, Seacliff
Court Hotel & Luxury Apartments, Seacliff Resort & Spa
Zanzibar, Serena Hotel, Southern Sun Dar es salaam, White Sands Hotel.
Black tomato, Boogle Woogle, Cultural Art Center,Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira.
Kwa
upande mwingine kutakuwa na kitengo cha Hosted Buyers Programme ambapo
Programme Maalum ya kuwatembeza mawakala wa Utalii katika maeneo Wageni
hao watatembelea Zanzibar , Lake Manyara na Ngorogoro.Lengo ni kuona,
kujifunza kuhusu utalii wa Tanzania, na kuonja (kuexperience ) ukarimu
wetu.
Pia
kutakuwa na kitengo cha Cultural Village ambalo ni Eneo lililotengwa kwa
ajili ya maonesho ambapo wajasirimali wadogo wataweza kuonesha bidhaa
na huduma zao.
Baadhi
ya bidhaa hizo ni kama Tinga Tinga, Wachongaji vinyago, watengenezaji
wa Sanaa mbalimbali, wanamitindo, vikundi vya burudani muziki wa bendi
na burudani (Utalii Band) na Kikundi cha utamaduni kutoka Chuo cha
Tumaini , Arusha .Pia kutakuwa na Nyama Choma (wageni wataweza kupata
vyakula vya kitanzania )
Kwa
ujumla TTB inawataka watanzania watembelee onesho hilo kutokana na
ukweli kwamba onesho la S!TE ni fursa ya kuhamasisha utalii wa
ndani,Watoa huduma mbalimbali za kitalii watakuwepo, wataweza kutumia
fursa hiyo kutoa maelezo kuhusu huduma zao na kuwahamasisha watanzania
kutembelea maeneo ya kitalii (vikundi mbalimbali vitawea kuhamasika
–wanafunzi, wafanyakazi nk)
Post a Comment: