MAGUFULI ATIKISA KAHAMA
Maelfu
ya Wakazi wa Mji wa Kahama na Vitongoji vyake wakimsikiliza Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dkt
John Pombe Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kujinadi kwa
kuwaomba wampigie kura ya ndio asubuhi na mapema Oktoba 25 mwaka huu
kwenye uchaguzi mkuu,ili aibuke mshindi na kupata ridhaa ya kuwaongoza
Watanzania katika awamu ya tano.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM
Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya Waananchi waliojitokeza
kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika katika viwanja vya CCM
mjini Kahama jioni ya leo.
Dkt.Magufuli leo amefanya mikutano yake ya kampeni katika wilaya za Mbogwe, Bukombe mkoani Geita na baadae halmashauri mpya ya Ushetu baadaye mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika mjini Kahama mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na umati wa watu uliorushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Star TV .
Akizungumza
katika mkutano huo wakati akiwaomba wananchi kujitokeza kwa
wingi Oktoba 25 mwaka huu kumpigia kura za ndiyo,Dkt Magufuli amesema
kuwa Serikali yake itashughulikia migogoro ya madereva na kuhakikisha
wanapata mikataba kutoka kwa waajiri wao ili kuboresha maslahi yao.
Amesema Madereva ni watu muhimu katika sekta ya usafirishaji na
wanafanya kazi ngumu,lakini maslahi yao hayatiliwi maanani,hivyo amesema
kuwa atahakikisha yanaboreshwa ili na waone faida ya kazi yao,na iwe
yenye kuthaminika ,hivyo serikali ya awamu ya tano itakayoongozwa na Dk.
John Pombe Magufuli italifanyia kazi ipaswavyo.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya
Bukombe mapema leo mchana,alipokuwa akielekea mkoani Shinyanga
kuendelea na kampeni zake za kuomba ridhaa kwa wananchi ya kuiongoza
Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano.
Mjumbe
wa kamati ya ushindi ya kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe
Magufuli,Mh.Samweli Sitta akiwahutubia wananchi wa mji wa Kahama jioni
ya leo kwenye mkutano wa kampeni za Urais,uliofanyika kwenye viwanja vya
CCM mjini humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu,Mh.Sitta a.k.a
Mzee wa viwango na kasi pia alimnadi Dkt Magufuli na kumwombea kura kwa
wananchi hao za ushindi na hatimaye akaibuke mshindi kwa nafasi ya Rais
na kupata ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika kipindi cha awamu ya
tano.
Maelfu
ya wananchi wa mji wa Kahama wakiwa wamekusanyika mkutano wa hadhara wa
kampeni,uliofanyika katika viwanja vya CCM mjini Kahama jioni ya leo.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwanadi Mgombea Ubunge wa Kahama
Ndugu Jumanne Kishimba pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Msalala
Ndugu Ezekiel Maige mbele ya maelfu ya wakazi wa mji huo kwenye mkutano
wa hadhara wa kampeni.
Wachimbaji
wadogo wadogo waishio eneo la Nyarugusu,Wilayani Geita wakimshangilia
mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mapema leo jioni alipokuwa
akielekea mkoani Shinyanga kuendelea na kampeni zake.
Post a Comment: