KUTOKA MAGAZETINI LEO
Magufuli: Watanzania tusidekezwe na utafiti
*Asema hawezi kuwa rais bila kupigiwa kura *Aanza kurusha makombora
Ukawa Na Bakari Kimwanga, Kahama MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amewataka Watanzania kutodekezwa na
matokeo ya utafiti unaoendelea kutolewa na taasisi mbalimbali. Kauli
hiyo aliitoa jana kwa nyakati tofauti, alipohutubia mikutano ya kampeni
iliyofanyika katika majimbo ya Busanda, Mbogwe ya mkoani Geita na
majimbo ya Ushetu na Kahama Mjini ya mkoani Shinyanga. Alisema katu
utafiti huo hauwezi kumfanya awe rais na hivyo ni lazima wana CCM na
Watanzania kwa ujumla wampigie...
Published By: Mtanzania
Lowassa kidedea
*Aongoza kwa asilimia 54.5 *Asema Serikali dhaifu imesababisha
migogoro NA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM UTAFITI mpya uliofanywa na
Taasisi ya Tanzania Development Initiative (TADIP) umeonyesha mgombea
urais wa Chadema, Edward Lowassa, angeshinda kwa asilimia 54.5 kama
Uchaguzi Mkuu ungefanyika ndani ya wiki tatu za Septemba mwaka huu huku
mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, angepata asilimia 40. Matokeo
ya utafiti huo yametolewa ikiwa ni siku chache baada ya wiki hii
Taasisi ya Twaweza kutoa matokeo ya utafiti wao yaliyoonyesha kama kura
zingepigwa Agosti na Septemba,...
Published By: Mtanzania Mgombea urais ampa ushindi Lowassa
Mgombea urais Chama cha Tanzania Labour (TLP), Macmillan Lyimo
amepingana na matokeo ya tafiti za kisiasa yaliyotongazwa hivi karibuni
na taasisi mbili, akisema kama Uchaguzi Mkuu ungefanyika Septemba,
mgombea urais wa Chadema na Ukawa, Edward Lowassa ndiye angeshinda kwa
kishindo....
Published By: MwananchiMAMBO MUHIMU AMBAYO LAZIMA UYAJUE KABLA YA MECHI YA SIMBA VS YANGA
Leo ni siku ambayo ilikuwa ikisubiriwa sana na mashabiki wengi wa
soka la Tanzania, leo ndio siku ambayo unapigwa mtanange wa Dar es
Salaam Darby (Yanga vs Simba) mechi hii inatajwa kuwa miongoni mwa Derby
kubwa barani Afrika lakini ikiwa ni Derby yenye upinzani mkubwa katika
ukanda wa Afrika Mashariki. Simba na Yanga zinakutana leo kwenye raundi
ya nne ya VPL lakini ikiwa ni mechi ya kwanza inayozikutanisha timu hizo
msimu huu, hapa chini nimekuwekea vitu muhimu unavyotakiwa kuvijua
kabla ya mechi haijapigwa ili wakati wa mchezo utapofika unakuwa
unajua...
Published By: Shaffih DaudaGharika ya Lowassa ndani ya mji wa Mererani, Simanjiro Mkoani Manyara jana
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa
Mererani, katika Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye uwanja wa
Machinjioni, Simanjiro Mkoani Manyara leo Septemba 25, 2015.Sehemu ya
Wananchi wa Mji wa Mererani, Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara
wakionyesha furaha yao mbele ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA
kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,
wakati akiwahutubia katika Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye
uwanja wa Machinjioni, Mererani, leo Septemba 25, 2015.Waziri Mkuu wa...
Published By: ZanziNews
Post a Comment: